Mwananchi aliyefika katika banda la Huduma ya Afya ya Macho akifanyiwa uchunguzi wa Macho katika maadhimisho ya sherehe za Nane Nane mkoani Lindi leo.
Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Lindi Dk.Mwita Machage akimpima mgonjwa wa macho wakati wa sikukuu ya Nane Nane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi leo.Huduma hii ya upimaji wa macho imefadhiriwa kwa ushirikiano wa shirika lisilo la kiserikali la Sightsavers Tanzania na sekretarieti ya mkoa wa Lindi Idara ya afya mkoa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mheshimiwa George B. Simbachawene alipotembelea banda la Sightsavers na idara ya afya mkoa akisikiliza kwa makini maelezo ya shughuli zinazofanywa na washirika hawa ili kutokomeza ugonjwa wa vikope mkoani Lindi hadi sasa jumla ya wagonjwa 830 wamekwisha pata usawaziswaji wa vikope mkoa wa Lindi. Katika wilaya ya Ruangwa na Nachingwea, kulia akizungumza Dr. Leonard Ndeki afisa mradi kutoka shirika la Sightsavers Tanzania katikati mwenye T-Sheti ya bluu ni Dr. Mwita Machage Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Lindi
Timu ya washiriki toka shirika la Sightsavers na watumishi wa Idara ya Macho Mkoa wa Lindi waliokaa wakiendelea kutoa huduma ya uchunguzi wa macho, Ushauri na Tiba kwa wananchi wa mkoa wa Lindi. Kutoka kushoto Dk. Mwita Machage, Dk. Leonard Ndeki (Sightsavers), Bw. Richard Shaban na aliyesimama mwenye T-Shirt nyeusi ni Zera Ombeni.
Baadhi ya wanawake na wanaume wa mkoa wa Lindi waliofika kwenye banda la Sightsavers na Idara ya afya mkoa kupata huduma ya macho wakisubiria kupata huduma wakisubiri kuhudumiwa na wataalam wa Macho.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mhe. Anne Makinda akifurahia jambo na Wataalam wa huduma ya Macho kutoka Sekretariet ya Afya Mkoa, Idara ya Macho na Sightsaver na wadau wa Mkoa wa Lindi walio katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa vikope chini ya ufadhiri wa mfuko wa Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Sightsavers Tanzania Bw. Gosbert Katunzi (kushoto) akionyeshwa na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Lindi baadhi ya picha na maelezo mbalimbali ya wagonjwa waliokwishapata huduma ya usawazishwaji na upasuaji wa mtoto wa jicho Mkoani Lindi kwenye banda la washirika kati ya Sightsavers na idara ya afya mkoa wa Lindi wakati wa maonyesho ya Nane Nane leo.
No comments:
Post a Comment