Friday, August 26, 2016

Programu ya LTSP kuvipatia Hatimiliki ya Ardhi Vijiji 37 vya MALINYI, KILOMBERO na ULANGA mkoani Morogoro



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume ya taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt Stephen Nindi ( Kulia ), akikabidhi Mpango wa miaka 20 wa Matumizi Bora ya Ardhi wa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mpango huo umelenga kutunza mazingira na Bio anuai Zilizopo nchini pamoja na kumnufaish Mwananchi wa Kipato cha kawaida.

Kiongozi wa Urasimishaji kupitia Programu ya LTSP, iliyo Chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi SAGWILE MSANANGA akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuwezesha Umilikishaji Ardhi kwa Wananchi pamoja na Vijiji Vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani MOROGORO.

Mratibu wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Wilaya za MALINYI, KILOMBERO na ULANG, Godfrey Machabe aliyevaa Tai Shingoni, akimsikiliza kwa Umakini Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Sagwile Msananga alipokuwa akielezea kuhusu Programu ya LTSP, kwa Washiriki wa Mafunzo ya Kuwezesha Umilikishaji wa Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani MOROGORO.

Kaimu kamishna wa Ardhi nchini Bi Mary Makondo ( katikati), akimsikiliza Katibu tawala wa Wilaya ya ULANGA mkoani Morogoro Ndugu Abraham Mwaivile aliyevaa Koti la Rangi ya Kijivu akisisitiza Jambo kwa Washiriki wa mafunzo ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Halmashauri hiyo, ambapo zoezi la Upimaji Mipaka ya Vijiji na Utoaji hatimiliki za Ardhi litafanyika.




Kiongozi wa Urasimishaji Sagwile Msananga kupitia Programu ya LTSP chini ya Wizara ya Ardhi inayoendelea katika Wilaya za MALINYI, KILOMBERO na ULANGA mkoani Morogoro akitoa Semina elekezi Juu ya Mradi huo, wenye lengo la Kutoa Kupika mipaka ya Vijiji na kutoka hatimiliki pamoja na kuhamasisha Ujenzi wa Masjala za Ardhi kwenye Vijiji.

Kiongozi wa Urasimishaji kupitia Programu ya LTSP, iliyo Chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi SAGWILE MSANANGA akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuwezesha Umilikishaji Ardhi kwa Wananchi pamoja na Vijiji Vilivyopo wilayani Kilombero Mkoani MOROGORO.

Picha zote na Hannah Mwandoloma

No comments: