Na Mwandishi wetu, Berlin
Nilipata kusoma habari
moja kutoka katika moja ya Vitabu vya Mwalimu Nyerere kuwa, Kijana anayetumia
pesa na Chakula cha Kijiji,akitumwa ughaibuni kutafuta kilicho chema,kisha
akapotelea huko asirejeshe chochote Nyumbani kwao,huyo atakua amefanya Uhaini.
Tunataka Vijana wanaokwenda Ughaibuni na kuleta Chakula
Nyumbani.
Nimelazimika
kuyakumbuka maneno haya baada ya kuona na kuskia habari za Petro Itozya Magoti
(pichani),Kijana wa Kitanzania aliyeko Ulaya (hususani ktk Nchi ya Ujerumani)
akihudhuria Mafunzo ya Uongozi na Mahusiano ya Siasa za Kimataifa.
Petro
Magoti amepata fursa ya kipekee ya kuwa Mwakilishi wa Tanzania ktk Mafunzo hayo
yanayohusisha Nchi 27 DUNIANI na ktk Bara la Afrika wametoka Vijana 14
pekee na kati ya hao Tanzania wamechaguliwa Vijana 2, kwa bahati mbaya kijana
mmoja hakuweza kuhudhuria kutokana na Majukumu aliyo nayo kwa sasa. Mafunzo
hayo ni ya siku 60,tangu Augst 4, hadi Octoba 4 mwaka huu.
Msingi mkubwa wa
Mafunzo hayo ni kuwaandaa Vijana katika Misingi ya Uongozi,pamoja na kujadili
namna ya kutumia Fursa zilizopo ktk Nchi husika ili kuwawezesha zaidi
kujiendeleza ktk Mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa,kuwa na uwezo mahsusi wa
kuzitumia Fursa zilizopo kwa Maendeleo ya Nchi zao.
Imepangwa
mafunzo hayo yafanyike ktk Majiji Makubwa manne Nchini Ujerumani ambayo ni
Berlin City, Humburge, Hannover na Munster, kisha Uholanzi ktk Majuma mawili ya
Mwisho.
Hii ni Fursa ya kipekee kabisa kwa Vijana wa Afrika na
hasahasa Tanzania kwani kupitia nafasi hiyo,licha ya kujifunza zaidi, Tanzania
tutakua Mwakilishi wa kuitangaza Nchi yetu katika maswala ya Uchumi, Siasa na
maswala ya Kijamii.
Kupitia Utangamano huo(Intergration) Tanzania inajipambanua
zaidi katika Fursa zake za Kibiashara na Kitalii. Hivyo ni Matarajio yetu kuwa
baada ya ukamilifu wa Mafunzo hayo kutafuatiwa faida kubwa zaidi za kiuchumi
ktk Nchi yetu kutokana na uwekezaji.
PETRO MAGOTI AKUTANA NA
KUFANYA
MAZUNGUMZO NA BILLIONEA KNOOP.
Katika kutekeleza
adhima ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifikisha Nchi katika Mapinduzi ya
Viwanda Vikubwa na Vidogo, Bwana Petro Magoti Mwakilishi pekee ktk Mafunzo hayo
Nchini Ujerumani amekutana na mmoja wa Wamiliki wakubwa wa Viwanda Vikubwa
Duniani Prof. KARL HEINZ KNOOP. Prof. Knoop anamiliki Viwanda ktk Nchi 17 Bara
la Ulaya na Nchi 4 Barani Afrika.
Katika
Mazungumzo yao,Prof. Knoop ambaye tayari ameonesha dhamira ya kuwekeza Nchini
Tanzania ktk Maeneo ya Himo huko Moshi pamoja na Kilindi-Tanga, amebainisha
dhamira yake ya kweli katika kuisaidia Serikali katika mpango wake huo wa
Kuifikisha Nchi ktk Viwanda ili kutatua Tatizo la Ajira kwa Vijana Tanzania.
Hata
hivyo, Prof. Karl Heinz Knoop ameeleza kuwa katika kutekeleza adhma yake hiyo
kwa wakati,amekutana na Changamoto lukuki katika ukubalifu wa kupewa Eneo la
Kujenga Viwanda Vikubwa vya Mashine za Kilimo kama vile Tractor, Mashine za
Kupanda, Kuvuna na kukausha mazao ya Shamba pamoja na Maghala makubwa ya
kuhifadhia Chakula.
Aidha, Prof. Knoop pia ameeleza dhamira yake ya kutaka
kujenga Kiwanda cha Kutengeneza Magari Makubwa ya Mizigo(Semi-Tralers) Nchini
Tanzania. Akifafanua zaidi, Prof. Knoop ameeleza kuwa Nje ya Changamoto hiyo ya
kupatiwa Eneo, alikusudia kufanya utekelezaji wa mpango wake huo mapema kadiri
itakavyowezekana ili kwenda sambamba na kasi ya Maendeleo ya Serikali ya awamu
ya tano.
Katika Maelezo yake kwa
Prof. Knoop, Bwana Petro Magoti, amemsihi na kumwomba Billionea Knoop kutokata
tamaa ktk dhamira yake hiyo ya kujenga Viwanda Tanzania kutokana Changamoto ya
kupata Eneo la Uwekezaji huo badala yake amemwomba kufika Tanzania ili Kuonana
na Mh. Rais ambaye kwake Viwanda ni kipaumbele kikubwa. Bwana Magoti amemweleza
kuwa,Mh. Rais wa Tanzania anavutiwa zaidi na wawekezaji walio tayari Kuijenga
Tanzania ya Viwanda ili kukuza Uchumi wake na kupunguza tatizo la Ajira hasa
kwa Vijana ambalo sasa ni kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Katika
mapendekezo yake, Bwana Magoti amemshauli pia Billionea Karl Knoop kujenga
Viwanda vyake ktk Mikoa ya Iringa na Morogoro ambayo ina maeneo mazuri kwa
Kilimo.
Baada
ya mazungumzo ya muda,Billionea Karl Heinz Knoop na Bwana Petro Magoti
wamekubaliana kuwa kati ya tarehe 17 hadi 22 OCTOBEE,2016.Prof. Knoop atafika
Tanzania kwa ajili ya kuonana na Mh. Rais ili kujadiliana nae juu ya Uwekezaji
huo wa Viwanda na zana za Kilimo. Pia Knoop ameahidi kutembelea Mikoa ya Iringa
na Morogoro ili kujiridhisha na maeneo hayo kwa ajili ya Uwekezaji ktk Viwanda
vya Kilimo.
Katika hatua nyingine
ya kuhakikisha kuwa fursa hiyo inatumika ipasavyo, Bwana Magoti amepata nafasi
ya kukutana na Wabunge Wastaafu na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ujerumani
wakiongozwa na Prof. Hemker anaetokana na Chama cha SPD pamoja na Wazee walioshiriki
ktk Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Katika
Mazungumzo yao, Viongozi hao kutoka Kada mbalimbali Nchini Ujerumani wamekubali
na kuahidi kuwa wako tayari kushirikiana na Rais wa Tanzania Dr. John Pombe
Magufuli Kujenga Viwanda Vingi kadiri watakavyopata Fursa na nafasi ya kufanya
hivyo.
Katika kutekeleza dhamira hiyo wameahidi kujikita katika kujenga Viwanda
vya Kutengeneza Mashine za Kupanda,kuvuna,kukausha Chakula,kuzalisha Mashine za
kupukuchua Mahindi na nafaka Mbalimbali pamoja na Maghara ya kuhifadhia
Chakula. Kwa kufanya hivyo watakua wametoa ajira nyingi kwa Watanzania ambao
kilimo ni sehemu kubwa ya Maisha yao.
Mafunzo ya Uongozi na
Mahusiano ya Siasa za Kimataifa yanaendelea hapa Ujerumani kwa Wiki ya pili
sasa.
Tunaamini kuwa yapo Mengi ambayo Mwakilishi pekee wa Tanzania atajifunza
kwa faida ya Nchi yetu. Lakini pia kutokana na jitihada zake, Tanzania
itatambulika zaidi na kujipambanua juu ya Fursa zilizopo Nchini kwetu na
kuwavutia zaidi Wawekezaji hasa ktk Sekta ya Kilimo na Viwanda. Ni katika hali
hii ndio hasa Uchumi wa Nchi yetu unaweza kufikia kuwa wa kati katika miaka hii
Mitano ijayo.
Ni
maombi yetu Watanzania kwa pamoja kuwa Mungu awaongoze Watanzania wote
wanaopata nafasi ya kuiwakilisha Nchi ktk Mataifa mbalimbali ili kuitambulisha
Nchi yetu na fursa zake ktk uso wa Dunia kwa faida ya Watanzania wote.
Nchi yetu itajengwa na
wenye Moyo.
Mungu awabariki sana!
#Berlin-Germany.
No comments:
Post a Comment