Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi kilichopo katika jimbo la Makunduchi Mkoa wa
kusini unguja, wamekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi, maarufu
kama kizimkazi day ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa nane.
Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho ambayo imeanzishwa na aliyewahi kuwa
mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi mhe. Samia Suluhu Hassan ambae sasa ni
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiadhimishwa
kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani, mashairi na michezo mbali mbali
ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata nafasi ya kuainisha changamoto
mbali mbali zinazo wakabili katika kijiji hicho.
Akimuwalisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amehaidi kutatua
baadhi ya changamoto zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho kwa
kushirikiana na mbunge wa jimbo la Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae
pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na
matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa
kuwa moja ya changamoto kijijini hapo.
Aidha, amewaahidi wana kizimkazi kuwa kwa kushirikiana na mbunge na uongozi wa
serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa ukihitaji matengezo nao utaanza
kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini hapo.
Wana Kizimkazi wamebainisha kukabiliana na changamoto itokanayo na mapato
na matumizi ya rasilimali ya bahari, pamoja na kupungua kwa nishati ya umeme
kutokana na ongezeko la mahitaji litokanalo na mji huo kupanuka.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri Mpina Pia alimuwailisha Makamo wa Rais
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kampuni inayotengeneza nishati ya
mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi itoknayo na taka za maganda ya
miwa na makarati na kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira
kwa kutokukata miti ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.
Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar ni Sehemu ya utekelezaji wa
majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Pamoja na kumuwakilisha Mhe,
Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi. Kizimkazi Day.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina aliyevaa suti akishika na kuangalia nishati ya mkaa unaotengenezwa na
malighafi itokanayo na taka za miwa na karatasi mjini Unguja, alipomuwakilisha
Makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kampuni ya Blue Spot,
inayotengeneza nishati hiyo bila kuharibu Mazingira.
Mabinti Mapacha Sabra na Sabrina Hassan wa shule ya sekondari makunduchi
wakitumbuiza kwa utenzi kwa meza kuu haipo pichani, wakati wa mkutano wa
Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina Hayupo pichani, kijijini Kizimkazi wakati wa siku ya kizimkazi ambapo
Naibu waziri Mpina alimuwakilisha Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la makunduchi.
Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina Pamoja na baadhi yaViongozi mbali mbali wa jimbo la Makunduchi
mkoa wa kusini Unguja, akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa jimbo hilo
katika kijiji cha kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama kizimkazi day,
alipomuwakilisha mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan aliyewahi
kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Aliyesimama katikati Mkurugenzi wa Kampuni ya Blue Spot Bw Buhet Juma ya
Mjini Unguja inayotengeneza nishati ya mkaa ambayo ni rafiki kwa mazingira
akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
aliyesimama kushoto, ambavyo nishati hiyo inavoengenezwa.
Naibu Waziri Mpina aliyesimama kati kati akishika chembe za malighafi
inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki kwa mazingira, alipotembelea kiwanda
kidogo cha Ble Spot Mjini Unguja kumwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Aliyekaa katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Ris Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina katika Picha ya Pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya
Makamu wa Raisi, Pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya kutengeza nishati ya
Mkaa rafiki wa mazingira, katika kiwanda cha Blue Spot. (Picha zote na Evelyn
Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
No comments:
Post a Comment