Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
waendesha Pikipiki/Boda Boda (hawapo pichani) kabla ya kuzindua Mashindano ya Mpira wa
Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo.
Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla
kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili
kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao. Kushoto ni Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kulia ni Wafadhili
wa Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi
mpira Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga
ikiwa ni ishara ya Naibu Waziri huyo kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa
Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo
yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo. Katika hotuba
yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria
za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali
mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao.
Sehemu ya waendesha Boda Boda jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati kiongozi huyo alipokuwa
anazungumza na madereva hao kabla ya kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa
Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini humo. Mashindano hayo
yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho. Katika hotuba yake, Masauni
aliwataka waendesha Boda Boda jijini Dar es Salaam na nchini kwa ujumla kufuata sheria za
usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali
mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akilionyesha Kombe
ambalo Mshindi wa Kwanza atakabidhiwa mara baada ya kumalizika Mashindano ya Mpira wa
Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni
ameyazindua mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiijaribu pikipiki mpya
ambayo atakabidhiwa Mshindi wa Kwanza mara baada ya kumalizika Mashindano ya Mpira wa
Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni
ameyazindua mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti)
akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed
Mpinga wakati alipokuwa anazungumza na Waendesha Boda Boda (hawapo pichani), kabla ya
Naibu Waziri Masauni kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki
katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Kamanda Mpinga
alisema Mashindano hayo ambayo yameshirikisha Wilaya za Temeke, Kinondoni na sasa Ilala
yanatarajiwa kumalizika Septemba 18, 2016. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
No comments:
Post a Comment