
Na Dixon Busagaga Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na serikali ya Korea ya Kusini imeanza mchakato wa ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kutunza taarifa za mienendo ya Wanyamapori kitakachojulikana kama Serengeti Internatinal Media Centre.
Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .
Tayari serikali ya Korea Kusini imeshatuma wajumbe wake kuja nchini tanzania kujionea eneo kitakapojengwa kituo hicho na kukamilisha taratibu nyingine muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung amesema mradi huo ni mwendelezo wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.
Akizungumza na ujumbe huo mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti Wiliam Mwakilema amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.
Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance amesema ujenzi utaanza mwezi october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi 14.












No comments:
Post a Comment