Saturday, August 13, 2016

Kambi tiba ya GSM yaokoa maisha ya watoto 12 jijini Mbeya, kuanza kazi Jumanne Iringa

 Na Mwandishi Wetu
Jumla ya watoto 30 wamehudhuria Kambi tiba ya GSM jijini Mbeya ambayo inaelekea katika kumaliza msimu wake wa pili, huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha vifo vya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi nchini, huku lengo kuu likiwa ni kutibia angalau watoto 400 katika kambi hiyo inayozunguka nchi nzima huku ikiwa imeshapita mikoa nane mpaka sasa.
Mkuu wa kambi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya MOI, Dk Othman Kiloloma, aliyeambatana na madaktari wenzake 10 wanaoshiriki kambi tiba hiyo amesema, tofauti na awamu ya kwanza, safari hii muitikio haukuwa mkubwa kutokana na sababu mbali mbali za kiutendaji lakini kubwa likiwa ni taarifa kuchelewa kuwafikia wananchi.
Dk Othman amesema kati ya watoto hao 30 waliohudhuria kambi tiba, 12 wamefanyiwa upasuaji, ambayo ndiyo tiba pekee inayotumika kuokoa maisha ya watoto waliokumbwa na ugonjwa wa vichwa vikubwa na mgongo wazi, huku wengine watatu wakihamishiwa katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Muhimbili, na wengine 15 wakipatiwa ushauri baada ya kugundulika kuwa umri wao hauruhusu kufanyiwa upasuaji huo.
Umri sahihi wa kuokoa maisha ya mtoto anayezaliwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi ni chini ya miaka mitano, ambaye bado fuvu la kichwa chake linakuwa bado halijakomaa na hivyo kumrahisisha mtoa tiba kupunguza maji yanayojaa kichwani kwa urahisi.
PICHANI JUU: Madaktari walioendesha zoezi la kuona watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi jijini Mbeya wakifurahia jambo wakati zoezi likiendelea, kutoka Kushoto ni Daktari Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dk  Lazaro Mboma, Daktari Bingwa wa Upasuaji ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kambi Tiba hii Hamis Shaaban,  Dk Benedict Austard, MwanaAbbas Sued, John Mtei na Siah Richard kutoka Taasisi ya Upasuaji na Mifupa MOI 


No comments: