Unao watoto wa namna mbalimbali. Unao uliowazaa ndani ya ndoa na wale uliowazaa nje ya ndoa. Unawapenda sana wote kwa usawa kwasababu wote ni watoto wako. Kuna suala la kifo na ungependa baada ya kifo chako watoto wako wote wafaidi kidogo ulichochuma. Lakini je hilo umelijengea mazingira.
Ni muhimu sana ujue kuwa suala la watoto wako kufaidi ulichonacho halitokani na matakwa yako, laa hasha bali linatokana na matakwa ya sheria. Wewe waweza kuamua watoto wako wote wa nje ya ndoa na wale wa ndani ya ndoa wapate mali lakini baadhi wakakosa kutokana na msimamo wa sheria.
Ni hapo unapotakiwa kuandaa mazingira yanayoendana na matakwa ya sheria ili watoto wako wote waweze kufaidi machumo yako.
1.FANYA HAYA ILI KUWAWEZESHA WATOTO WA NJE YA NDOA KURITHI.
a. KWA WAISLAMU.
Kama wewe ni muislam na una mtoto/watoto nje ya ndoa hakikisha unaandika wosia ambao utampatia mali hata huyo mtoto wa nje ya ndoa. Lakini lazima ujue kuwa mali yako yote uliyonayo ni 3/3 = (100%). Hivyo 2/3 ya mali yote ni lazima iende kwa warithi halali ambamo mtoto wa nje ya ndoa hataingia kabisa. Katika mali hiyo ya 2/3 wala haihitaji wosia kwakuwa tayari sheria ya kiislam imeeleza vipi hiyo mali igawanywe.
Uhuru wako wa kugawa mali kwa wosia upo katika 1/3 basi na si vinginevyo. Na ni kusema kuwa mtoto/watoto wa nje ya ndoa haki yao ipo katika 1/3 tu. Ikiwa utampatia mali zaidi ya 1/3 basi anaweza kunyanganywa . Kwahiyo uelewe kuwa wosia utakaoandika unahusu 1/3 ya mali tu.
Zingatia kuwa usipoandika wosia kugawa 1/3 yote au sehemu yake kwa mtoto/watoto uliowazaa nje ya ndoa basi hawatapata mali kabisa baada ya kifo chako. Na hii ni kwasababu watoto hao hawaruhusiwi kurithi kisheria. Kwahiyo utaona kuwa unachotakiwa kufanya ili hao watoto wasikose ni kupiga hesabu ili kupata 1/3 ya mali yako na kuwapa yote au sehemu yake.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
No comments:
Post a Comment