Sunday, August 7, 2016

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga katika jiji la Mwanza wamegoma kutii agizo la uongozi wa jiji la kuwataka kuhama katikati ya jiji hilo. https://youtu.be/ZAGa1VONGU0

SIMU.TV: Serikali imesema inatarajia kutenga eneo na kutengeneza soko katika mpaka wa Tanzania na Zambia ili kuwawezesha watanzania kufanyabiashara na kulinda usalama. https://youtu.be/RJWhdpWiZaA

SIMU.TV: Chama cha demokrasia na maendeleo mkoani Rukwa kimetangaza kuunga mkono tamko la kamati kuu ya chama hicho la kuendesha operesheni UKUTA. https://youtu.be/k99NYCTZwTo

SIMU.TV: Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr John Pombe Magufuli leo ametembelea makanisa na misikiti katika wilaya ya chato na kuwasihi wananchi kuendelea kuliombea taifa. https://youtu.be/dJbBi2zhcY4

SIMU.TV: Wakulima wengi hawajafikiwa na elimu ya kilimo bora licha ya wananchi wengi hapa nchini kutegemea kilimo kama njia kuu ya kujipatia kipato. https://youtu.be/WZOaZ-_G8aU

SIMU.TV: Kamati ya viongozi wa dini ya mkoa wa Dar es Salaam imetayarisha kitabu cha kupinga mauaji ya tembo kwa kushirikisha vitabu vitakatifu vya dini zote. https://youtu.be/AoRwxxEKMgI

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameongoza waombolezaji kwenye mazishi ya Sheikh wa wilaya ya Temeke Sheikh Mohamad Mshindo. https://youtu.be/FxUkGg3PvW8

SIMU.TV: Timu ya Simba kesho inatarajia kufanya tamasha lake la kila mwaka maarufu kama Simba day ambapo watawatambulisha wachezaji wao wapya. https://youtu.be/8X0sp2tJCMU

SIMU.TV: Wafanyabiashara wa filamu za nje wamekutana na mbunge wa Ilala Hassan Zungu wakimuomba kuwakutanisha na waziri wa habari sanaa na michezo ili kutatua matatizo yao. https://youtu.be/Mzt-gD5n8Lk

SIMU.TV: Umoja wa kukuza vipaji pamoja na kuendeleza sanaa kata ya Mabwepande wamewaomba wananchi wa jiji la Dar es Salaam kuitikia agizo la rais la kufanya usafi na kutunza mazingira. https://youtu.be/_82XksXezpw

SIMU.TV: Timu ya Liverpool imeonesha kukomaa katika maandalizi ya ligi kuu Uingereza baada ya hapo jana kuitandika klabu ya Barcelona kwa magoli manne kwa bila. https://youtu.be/edpU40A8CRM

No comments: