Tuesday, August 30, 2016

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Watu watatu wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka mkoani Tanga; https://youtu.be/pgAaeT-MZhs

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli, amewaalika wawekezaji kutoka nchini Cuba pamoja na serikali ya nchi hiyo kuja kuwekeza nchini Tanzania katika viwanda vya sukari na dawa za binadamu; https://youtu.be/JMczzQHQUYE

SIMU.TV: Watoto wawili wamekufa na mmoja kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari walipokuwa wanavuka barabara kuelekea shuleni eneo la Kibonde maji, Mbagala jijini Dar Es salaam; https://youtu.be/LTxzrVWnYwk

SIMU.TV: Mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC rais wa Botswana ametoa pongezi kwa rais wa Tanzania Dr Magufuli kwa kuchaguliwa kuingoza Tanzania; https://youtu.be/ONtm1fY5irA

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi wa eneo la Unga Limited mkoani Arusha, wamepinga kufanya maandamano Septemba 1na kusema kuwa hawako tayari kuvuruga amani ya nchi;https://youtu.be/qk1q0IOxE5c

SIMU.TV: Katibu wa Chadema mkoani Mwanza John Mzwalile, amekihama chaka hiko na kuhamia CCM kutokana na kile alichokisema kuchoshwa na ubabaishaji ndani ya chama hicho; https://youtu.be/C1FvLwxz93A

SIMU.TV: Maandalizi ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua katika eneo la Ludewa mkoani Mbeya, yamekamilika na wananchi wanakaribishwa kwenda kushuhudia tukio hilo la kihistoria; https://youtu.be/_-s6nkKEB78

SIMU.TV: Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ limewatoa hofu watanzania kwa shughuli zake mbalimbali ambazo litazifanya siku ya tarehe 1 mwezi septemba;https://youtu.be/kiNZbxiOlS4

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa amesema serikali imejipanga kulifufua kikamilifu shirika la ndege nchini ATCL;https://youtu.be/mGrM_irIaUI

SIMU.TV: Shirika la reli nchini TRL limesema limeamua kupandisha nauli kwa usafiri wa treni kutoka Stesheni mpaka Pugu kutokana na umbali wa vituo hivyo;https://youtu.be/mhuM-zFmgzw

SIMU.TV: Wananchi mkoani Tanga wameamua kushirikiana kulinda mipaka yao ili kudhibiti ongezeko la bidhaa bandia kutoka nchi jirani; https://youtu.be/-x3w1k-OS2k

SIMU.TV: Waziri wa Habari Nape Nnauye amesema mashindano ya michezo ya walimu walioko kusini mwa Afrika yataongeza mshikamano na umoja baina ya nchi husika;https://youtu.be/q7yrCPIG1_8

SIMU.TV: Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Polisi Dodoma kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa mkoani humo;https://youtu.be/D3Mlfyi4o4Y

SIMU.TV: Mashindano ya wazi ya Gofu yatakayofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Lugalo, yatatumika kuchagua timu ya taifa itakayokwenda kushiriki mashindano ya Afrika mashariki; https://youtu.be/ERp8rmi1AtU

SIMU.TV: Bendi mpya ya muziki ya Dar Musica itazinduliwa wiki hii katika ukumbi wa Mango Garden huku wenyewe wakiahidi kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wao;https://youtu.be/UsBHtyZUVHY

No comments: