Thursday, August 11, 2016

DCB WATOA MSAADA WA MADAWATI 100 KATIKA SHULE YA MSINGI MSUFINI JIJINI DAR LEO.

DCB Commercial Bank wametoa Msaada wa Madawa 100 kwa shule ya Msingi Msufini iliyopo Kata ya Chamanzi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza katika Hafla Fupi ya Kukabidhi madawati katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mipango na Uvumbuzi wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo amesema kuwa benki hiyo imeunga mkono jitihada ya serikali katika upungufu wa Madawati shuleni benki hiyo imetoa madawati 100 kwa Manispaa ya Temeke katika shule ya Msingi Msufini.

Na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalla Chaurembo amewashukuru benki ya DCB kwa kutoa mchango huo hasa katika shule ya Msingi Msufini yenye changamoto kubwa ya ongezeko la watoto kwa kila mwaka.

Pia amewaomba makampuni Mengine yajitokeze kuchangia katika shule hiyo kwani inachangamoto ya ukosefu wa Kisima cha maji pamoja na Madawati.

Kwa Upande wa wanafunzi wa shule hiyo wamewashukuru benki ya DCB kwa kupunguza Mzigo wa Upungufu wa Madawati katika shule hiyo kwani kwa sasa watakuwa wanakaa kwenye madawati.

 Mkuu wa Mipango na Uvumbuzi wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati katika chule ya Msingi Msufini iliyopo kata ya Chamanzi wilayani Temeke jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Mipango na Uvumbuzi wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalla Chaurembo madawati 100 ya shule ya Msingi Msufini jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Mipango na Uvumbuzi wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo akitoa mkono wa shukrani mara baada ya kukabidhi madawati kwa shule ya msingi Msufini jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Mipango na Uvumbuzi wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo (Kutoka Kulia wa Pili) akiwa amekaa kwenye dawati ambalo limekabidhiwa leo katika shule ya Msingi Msufini wakwanza kulia ni Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalla Chaurembo wakiwa kwenye picha ya Pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
 Mkuu wa Mipango na Uvumbuzi wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo (Kutoka Kulia wa Pili) na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdalla Chaurembo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazazi pamoja na wajumbe wa bodi ya chule mara baada ya kukabidhi madawati katika shule ya msingi Msufini jijini Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya DCB jijini Dar es Salaam leo. 

Diwani wa Kata ya Sandali na Mwenyekiti wa Huduma za Uchumi, Elimu na Afya katika shule ya Msingi Msufini, Abel Tarimo akizungumza wakati wa kukabidhiwa madawati ya shule ya Msingi Msufini jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wafanyakazi wa DCB wakiteta jambo.


No comments: