Monday, August 29, 2016

AIRTEL MONEY TIMIZA YAFANYA SEMINA NA MAWAKALA MKOA WA MWANZA

Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitia msisitizo zaidi katika semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
Mawakala toka viunga mbalimbali ndani ya jiji la Mwanza wamekusanyika hapa ndani ya ukumbi wa Gold Crest Hotel kwa nia ya kupata mafunzo.
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.'MUDA NI MALI' = Jinsi Airtel Money Timiza inavyokomboa muda huku ikimkuza na kumnyanyua mwananchi toka lindi la umasikini.
David Wankuru ambaye ni Meneja wa Airtel Mkoa wa Mwanza akifafanua kilichofanyika ndani ya semina kwa mawakala, masharti na masuala yote juu ya Airtel Money Timiza.
Ni sifa zipi zitampa mteja fursa ya kuweza kukopeshwa na Airtel Money Timiza? Joel Laizer ambaye ni Meneja wa Mauzo Airtel Mwanza anafunguka zaidi.
Mawakala - Kalunde Kafiti na wenzake hapa wanafunguka mengi juu ya 1.Wazo la Airtel Timiza linamanufaa gani kwa wenye kufanya kazi ya miamala? 2. Nini Tahadhari kwa matapeli wanaoweza kuitumia Airtel Money Timiza kufanya yao? 3.Jeh Mikopo itawasaidiaje wajasiliamali ambao suala la mtaji limekuwa changamoto kubwa kwao?

No comments: