Friday, July 15, 2016

ZUNGU AMKABIDHI MAKONDA HUNDI YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 27, MADAWATI 30

 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh. Mussa Zungu (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yenye thamani ya Sh. Milioni 27, sambamba na kukabidhiwa madawati 30 kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa karume, Haji Bechina (kulia) yenye thamani ya milioni 36, hafla hiyo ilifanyika Mtaa wa Karume, Jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji .
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamMh.  Paul Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa hafla ya kukabidhiwa mfano wa hundi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu yenye dhamani ya Sh. Milioni 27 kwa niaba ya uchangianji wa madawati kwa kuitikia wito wa Rais Magufuli na katika hafla hiyo mwenyekiti wa Mtaa wa Karume,  Haji Bechina na yeye alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam madawati 30 yenye dhamani ya Sh. Milioni 36.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume,  Haji Bechina akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mh. Paul Makonda mara baada ya hafla ya kukabidhiwa hundi ya milioni 27 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala,  Mh. Mussa Zungu na kupokea madawati 30 yenye dhamani ya Milioni 36 kutoka kwa Mwenykiti huyo.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akizungumza katika hafla hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa karume, Haji Bechina na kuanzia kushoto ni Diwani wa Kata ya Ilala Saady  Khimji  na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh. Mussa Zungu.
 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akizungumza jambo katika hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume,  Haji Bechina (kushoto) akimtambulisha Magreth Mwandri (wa pili kushoto) kwa Mh. Paul Makonda ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa Mtaa Karume na sasa amehamishiwa Kata ya Kitunda Mtaa wa Kitunda Kati
Mh. Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda akiagana na wananchi mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye dhamani ya Sh. Milioni 27,na Mbunge wa Ilala Mussa Zungu na kupokea madawati 30 yenye dhamani ya Milioni 36 toka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Karume.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa karume, Haji Bechina (kulia) akimpokea Mkuu wa Mkoa Paul Makonda wakati alipofika katika hafla ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 27 na Mbunge wa Jimbo la Ilala na kupokea madawati 30 yenye dhamani ya Sh. Milioni  36 kutoka kwa Mwenyekiti huyo 




 Wananchi wakiwa katika hafla hiyo

  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 

No comments: