Saturday, July 9, 2016

WHITEDENT WASHEREKEA MIAKA 25, WAZINDUA MCHEZO WA BAHATI NASIBU JIJINI DAR LEO.

KAMPUNI ya Chemi & Cotex inayotengeneza bidhaa za za afya ya Mdomo ya Whitedent imezindua mchezo wa bahati nasibu wa kujishindia moja ya magari 25 aina ya Suzuki Alto K10 jijini Dar es Salaam leo.

Bahati nasibu hiyo imezunduliwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru wakati wa kusherehe madhimisho ya  miaka 25 ya Whitedent jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa  Kiwanda cha Chemi & Cotex kimeadhimishi miaka yake 25 kuwaajili ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. 

Nae Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan amesema kuwa katika kusherekea miaka 25 ya bidhaa ya Whitedent wametaka kuwashirikisha wananchi wote katika mafanikio ya kampuni yao.

Amesema kuwa wananchi watawashirikisha kwa kuchezesha baahati nasibu hiyo ili kujipatia zawadi ya gari ambayo ni Mpya kwa kuotea ndani ya gari kuna maboksi mangapi kwa kujaza fomu ya kushiriki katika shindano hilo.

Mafanikio makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa uwezo wa Viwanda hapa nchini ni mkubwa tunauwezo wa kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa watanzania kwa bei nafuu na pia kuuza ulimwenguni kote. amesema Swaminathan

Shindano hili lililozinduliwa leo jijini Dar es Salaam pia limezinduliwa katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Musoma pia wanategemea kuzindua katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,Morogoro na Kigoma katika kusherekea miaka 25 ya Whitedent hapa nchini.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini Dar es Salaam leo ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia idadi ya Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan akizungumza wakati wa sherehe za kusherekea kutimiza miaka 25 ya kampuni ya Whitent iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni Chemi & Cotex, M Balasubramanium akizungumza wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini Dar es Salaam leo ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia idadi ya Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan  wakifurahia jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru wakati wa kusherekea miaka 25 ya whitedent jijini Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Chemi& Cotex wakiwa katika sherehe ya kusherekea miaka 25 ya Whitedent iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru akiweka maboksi ya Whitedent katika gari jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya washiriki wa shindano hilo kubashiri katika mchezo wa bahati nasibu kujua kama kuna boksi ngapi katika kila gari ambalo limewekwa maboksi hayo. 


 m
 Kikundi cha ngoma wakitumbuiza wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini Dar es Salaam leo ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia idadi ya Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
 Baadhi ya wanakikundi wakiigiza igizo wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent jijini Dar es Salaam leo.

No comments: