Friday, July 15, 2016

WAZIRI NAPE AANZA KULA SAHANI MOJA NA WAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHINI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika Operesheni ya kuwasaka waharamia wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini, hali inayopelekea wasanii hao kazi zao kuzorota. Waziri Nape leo ameianza Operesheni hiyo kwa kutembelea Maduka mbalimbali yaliopo eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akisimamia zoezi la ukusanyaji wa kazi zilizodurufiwa na wafanyabiashara hao katika moja ya Maduka yaliopo eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimsiliza mmoja wa watuhumiwa wa kudurufu kazi za wasanii, aliekuwa na mitambo ya kufanyia kazi hizo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakati wa Operesheni ya kuwasaka wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.No comments: