Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi wa Kampuni
ya Uchimbaji Madini ya mkoani Geita (GGM) pamoja na Viongozi wa Serikali wa mkoa huo,
kuhusiana na masuala mbalimbali ya utatuaji wa migogoro iliyopo kati ya GGM na wananchi
wanaoishi jirani na mgodi huo. Waziri Mwakyembe aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, katika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo
katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati),
na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto) mara baada ya
kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi zilizofanywa na viongozi hao wa Wizara.
Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM), Terry MulPeter
akizungumza katika kikao kati ya uongozi wa kampuni yake na viongozi wa serikali uliokuwa
unaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hawapo pichani). Kikao hicho kilifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo
katika kikao cha viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya
Geita (GGM) cha kujadiliana masuala mbalimbali ya utatuzi wa migogoro kati ya kampuni hiyo
na wananchi wanaoishi jirani na kampuni hiyo. Kikao hicho ambacho kiliongozwa na Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wanne kulia) ambacho kilifanyika katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Geita. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel
Kyunga. Wa pili kulia ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia), Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kushoto kwa Dk Mwakyembe), Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati ya Dk Mwakyembe na Mkuu wa
Mkoa) pamoja na viongozi wengine wakitoka kulikagua Bweni la Mahabusu la Gereza Chato
linalojengwa mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo
ndani ya Bweni la Mahabusu la Gereza Chato linalojengwa mkoani Geita. Wapili kulia ni Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huo.
Kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Edward
Kaluvya.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari
mjini Chato, mkoani Geita mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yao na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto). Katika ziara yao licha ya
kufanya majukumu mengi ila walifanikiwa kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya
Uchimbaji Madini mkoani Geita (GGM) na pia walilikagua Gereza Chato linalojengwa mkoani
humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment