Wednesday, July 6, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAONGOZA WAUMINI WA KIISLAM KATIKA SWALA YA EID-EL-FITR ILIYOSWALIWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Mufti wa Tanzania, Alhaj Sheikh Abubakary Zubeir (katikati), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum pamoja na Naibu Mufti, Sheikh Hamid Jongo katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum akitoa hotuba ya Eid El Fitr, kwa waumini wa Dini ya Kiislam walioshiriki ibada hiyo, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salam za Eid El Fitr, kwa waumini wa Dini ya Kiislam walioshiriki ibada hiyo, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kulia) akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, wakifatilia kwa makini hotuba ya Eid El Fitr, iliyokuwa ikitolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Alhaj Mussa Assad akijumuika na waumini wenzake katika Swala ya Eid el Fitr, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam kutoka maeneo mbalimbali wakijumuka pamoja katika Swala ya Eid el Fitr, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipeana Mkono wa Eid el Fitr na Mufti wa Tanzania, Alhaj Sheikh Abubakary Zubeir, mara baada ya Swala, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiendela kupena mikono na waumini wengine.
Dua ya pamoja.No comments: