Friday, July 8, 2016

WASHINDI WANNE WANYAKUA ZAWADI KATIKA KAMPENI YA FAIDIKA NA AMANA BANK

Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi,Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo .
Zawadi ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE (Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo. 
Mshindi wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia.Pichani ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi za kitanzania Million Tano 

Katika kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha maonyesho ya saba saba Tarehe 7/7/2016.

Wateja hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.

Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama Luninga,Jokofu,Microwevu,Pamoja na Table Feni yenye AC Pia.
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa 

Akizungumza na wanahabari mapema leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi hao meneja masoko wa Bank hiyo Ndugu DASSU MUSSA amesema kuwa bank ya amana imejipanga kuendelea kuwafikia na kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao mbalimbali,huDuma pia ambazo zinafwata misingi ya sheria ya kiislamili kuwapatia faida iliyo halali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.

Aidha amewahamasisha watanzania wote kujijiengea na kudumisha utamaduni wa kujiwekea akiba ya pesa kwa ajili ya malengo mbalimbali katika benk ya amana ili wapate kufurahia huduma bora zitowelewazo kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.
Meneja masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea ukingoni 

Ameongeza kuwa kampeni ya faidika na amana bank ni mwanzo tu wa kampeni za bank hiyo zitakazohusisha wateja kuweka fedha na kujishindia zawadi mbalimbali kutoka amana bank ukiachia faida nyingine zipatikanazo kwa wateja kujiwekea akiba huku akisema kuwa wanatarajia kutangaza kampeni nyingine kubwa itakayowezesha wateja wengiine Zaidi kujishindia zawadi lukuki kutokana na kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba zao amana Bank Bank ambayo inafwata misingi ya kiislam kikamilifu.
Zawadi ambazo zimetolea kwa washindina Bank ya Amana ambazo jumla zimegharimu kiasi cha shilingi million Tano 


Aidha akiwahamasisha watanzania kujiunga na Bank hiyo amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa wakidhani Bank hiyo ni kwa ajili ya waislam jambo ambalo sio kweli huku akitanabaisha kuwa Bank hiyo inahusisha wateja wa Dini zote bila kubagua hivyo watanzania wajiunge kwa wingi katika Bank hiyo,

Washindi waliojishindia zawadi mbalimbali katika hitimisho la Kampeni hiyo ya Faidika na Amana Bank ni pamoja na Pikira Nlongane aliyejishindia zawadi ya Televission kwa kuwa mshindi wa kwanza,Shakira Ibrahim aliyeshika nafasi ya pili na kujishindia zawadi ya Friji kubwa,Khamis Said aliyejishindia Microwave huku mshindi wa nne akiwa ni Hemed Suleiman aliyejishindia Table Feni katika droo hiyo.
Picha ya Pamoja maafisa wa Bank ya amana wakiwa na washindi wa Zawadi mbalimbali za kampeni ya Faidika na Amana Bank mara baada ya utoaji wa zawadi hizo katika maonyesho ya Saba saba 

Bank ya amana ni bank inayoongozwa kwa ustadi mkubwa na misingi ya Dini ya kiislam huku ikiwahudumia watanzania wapatao Elfu 34 katika matawi yake saba nchi nzima hadi sasa.

No comments: