Wednesday, July 27, 2016

WASHINDI WA PROMOSHENI YA TUSKER FANYA KWELI UWINI WAKABIDHIWA MPUNGA WAO



Dar es Salaam; 26 Julai, 2016, Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia promosheni yake ya Tusker Fanya Kweli Uwini iliyomalizika wiki iliyopita imeendelea kuwakabidhi washindi wa promosheni hiyo vitita vyao kutoka mikoa mbali mbali nchini. Mwishoni mwa wiki baadhi ya washindi hao walikabidhiwa pesa zao katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa washindi wakishindwa kuficha hisia zao juu ya swala hilo.

Hafla hiyo iliyopambwa na burudani mbalimbali ya muziki ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, wapenzi na watumiaji wa bia ya Tusker pamoja na viongozi mbalimbali wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.

“Leo mbele yenu tumewakabidhi washindi wetu pesa zao za ushindi Milioni moja kila mmoja walizoshinda katika droo tulizochezesha tunaimani watatumia katika masuala ya kimaendeleo. Kuwapongeza sana washindi wetu wote na kwa nanma ya pekee hawa tuliowakabidhi pesa zao joini ya leo pia nawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono siku zote kwani wao ndio waliotuwezesha sisi kufika hapa leo.” Alisema Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile.

Naye mmoja wa washindi waliokabidhiwa Milioni moja Juliana Petro Mwasigara aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Tusker kwa kumpatia pesa hizo na kueleza namna atakavyoitumia. “Nashukuru sana pesa hii itanisaidia mimi na familia yangu kwani nina watoto wananitegemea na sina mume, hivyo kwangu hii ni kama miujiza bado”, alisisitiza Juliana.

“Mimi nafanya biashara ya karanga lakini kwa pesa hii niliyopokea leo ntabadilisha biashara mana nimepata mtaji wa kutosha nafikiria kununua pikipiki niingie barabarani, bado siamini naangalia simu yangu kila wakati kuhakikisha ujumbe mfupi nilioupata wa kupokea Tsh 1,000,000.” Alieleza mshindi wa pili Ally Mkemi.

Washindi waliokabidhiwa pesa zao katika hafla hiyo ni Juliana Petro Mwasigara, Inai Ngwavi na Ally Mkemi wote kutoka Dar es Salaam. Bado washindi mbalimbali wa promosheni hiyo wanaendelea kupokea vitita vyao huku ikiwa tayari droo zote zimeshakamilika wiki iliyopita.

‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ ni promosheni iliyoanza takribani wiki tisa zilizopita mikoa yote nchini na leo imekamilisha washindi 100 na kufungwa rasmi kwa droo za promosheni hiyo.
 Meneja Mauzo wa Eneo Erick Pallangyo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Tsh Milioni moja mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini Juliana Petro Mwasigara (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam  

  Meneja Mauzo wa eneo Erick Pallangyo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Tsh Milioni moja mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini Inai Ngwavi (kulia) 
 Mmoja ya wageni waalikwa Juma Ramadhani (katikati) akisoma ujumbe mfupi wa maandishi unaoonesha pesa iliyoingia kwa Ally Mkemi (kulia) mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, kushoto ni Meneja Mauzo wa eneo(Area Sales Manager) Erick Pallangyo (kushoto).
 Mmoja wa washindi wa Tusker Fanya Kweli Uwini Ally Mkemi(kulia) akionesha msg ya pesa aliyoshinda, pembeni yake ni Meneja Mauzo wa Eneo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.
  Kikundi cha burudani cha amsha amsha kikitoa burudani wakati wa hafla ya makibidhiano kwa baadhi ya washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments: