Saturday, July 30, 2016

Wasanii waaswa kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zao

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kulia) wakati wa hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akizungumza jambo na wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kushoto) na Bw. Darish Pandit(wa pili kushoto) wakati wa hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo na kulia ni mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment Bw. Hanscana. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua studio mpya ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kushoto ni mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Studio Bw. Darish Pandit(kushoto) kwa kuhusu maeneo mbalimbali ndani ya studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akiangalia moja ya vyumba vya kurekodia na kutengengeneza video vilivyopo ndani ya studio ya Wanene Entertainment mara baada ya kuizindua studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyekaa) akiangalia moja ya ya kazi zilizorekodiwa na kutengenezwa na kampuni ya Wanene Entertainment Studio wakati alipokuwa akizundua studio hiyo iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam Julai 29, 2016. 
Mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment Studio Bw. Hanscana akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyekaa) naamna kazi za video zinavyotengenezwa mara baada ya kurekodiwa katika maeneo mbalimbali alipotembelea studio hiyo mara baada ya kuizindua rasmi Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo akizungumza wakati wa hafla uzinduzi wa studio za kisasa za Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa studio yake uliofanya na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa studio za kisasa za Wanene Entertainment na wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo na kulia ni Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Musa Nyoni.
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi


Wasanii nchini wameaswa kuzingatia maaadili katika utengenezaji wa kazi zao ili kuenzi na kulinda mila, desturi na tamaduni za mtanzania.

Wito huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati akizindua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ya Wenene Entertainment.

Mhe Anastazia Wambura amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa hawafati maadili katika utengenezaji wa kazi zao na kuvifanya vyombo vinavyosimamia kazi za sanaa nchini kama Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutoa adhabu dhidi yao kutokana na ukiukwaji wa maadili katika kazi zao.

“Ninaiomba kampuni ya Wanene Entertainment kuisaidia Serikali kuwaelimisha wasanii watakaoleta kazi zao kutengenezwa kwenu kuzingatia maadili badala ya kutengeneza kazi ambazo haziendani na maadili ya nchi yetu” alisema Mhe Anastazia.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo amehaidi kushirikiana na studio ya Wanene Entertainment kuendeleza sanaa ya Tanzania kufikia katika viwango vya kimataifa na kuongeza pato la wasanii na taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Wanene Entertainment Bw.Darsh Pandit amesema kuwa ufunguzi wa studio hiyo ni muitikio wao kwa Serikali ya awamu ya tano katika suala la kutoa ajira kwa vijana na kuwezesha vijana kujiajiri kwa kutumia vipaji vyao kupitia kazi za sanaa.

“Studio hii ina lengo la kukuza na kuendeleza sanaa ambayo imekuwa ajira kubwa kwa vijana wengi na tunaahidi kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zetu na pia tutazingatia ubora ili kuitangaza sanaa ya Tanzania kimataifa” alisema Bw. Pandit.

Aidha mtayarishaji wa video katika kampuni hiyo Bw. Hasacna amesema kuwa ni fursa sasa kwa watayarishaji wa video wanaochipukia nchini kuonesha vipaji vyao kwa kuwa wabunifu katika uandaaji na utengenezaji wa video za muziki na filamu kwa ujumla.

No comments: