Wednesday, July 20, 2016

WAKUU WA IDARA NDANI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA WAMEUNGANA NA MBUNGE WA JIMBO LA MKURANGA ABDALLAH ULEGA KUFANYA ZIARA YA KUKAGUA NA KUANGALI KERO WANAZOKUTANA NAZO WANANCHI.

 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibesa katika ziara ya kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi akiwa ameambatana na wakuu wa idara mbalimbali  ndani  ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga  leo Julai 19, 2016 katika Kijiji cha Kibesa wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
 Wananchi wa kijiji cha Kibesa wakimsikilza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega leo Julai 19, 2016 katika Kijiji cha Kibesa wilaya Mkuranga mkoani Pwani. 
Sehemu ya  wakuu wa Idara  malimbali ndani ya  Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakuu hao ambao wengi wao ni wapya kwenye wilaya hiyo wanashiriki kikamilifu  kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kibesa.
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akichangia fedha taslimu shilingi laki tatu na nusu Kwa ajili ya kununua Betri ya Solar power, kushoto ni Mwenyekiti wa  serikali ya kijiji cha Mbezi   Muungwana, Hassan Abdalla.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akimetembelea shule ya msingi Mbezi   kushoto  kwake anayempa maelezo ni Mwenyekiti wa  serikali ya kijiji cha Mbezi   Muungwana, Hassan Abdalla  
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii).

WAKUU wa Idara ndani ya  Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wameungana na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega kufanya ziara ya kukagua  na kuangali kero wanazokutana nazo  wananchi ili  kuweza kuzitatua.

Jimbo la Mkuranga limekuwa na changamoto kubwa huku wananchi wakilalamikia zaidi miundombinu mibovu ya barabara,Zahanati,Maji safi,pamoja na uvamizi wa ng,ombe kwenye Mashamba ya wakulima.

Akizungumza kwaniaba ya wakuu wa Idara wengine Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo Kanyala Mahinda  alisema katika ziara hizo ambazo anazifanya Mbunge na kuwashirikisha wao ni jambo jema mno. 

Alisema kuwa kuzunguka kwako kunawapa  uzoefu wa kujuwa mazingira ya wilaya hiyo lakini pia kutambua kero za moja Kwa moja ambazo wanakabiliana nazo.

"Mbunge anafanya jambo jema  la kuamua kuambatana nasi kwani ukizingatia watumishi waliwengi ni wageni ndani ya Mkuranga hivyo nasi tunapata mengi ikiwa pamoja na kuona kile kilichohaidiwa Kwa wananchi."alisema Mahinda.

Naye Mbunge  Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibesa alisema kuwa amelazimika kupita kutoa shukrani kwa wananchi wake hususani  Kwa Kazi kubwa waliyoifanya ya kukichagua cha Mapinduzi na yeye kumpa heshima ya ubunge.

Pia alisema kuwa ni wachache ambao wakipata wanakumbuka kurudi kwani hivi sasa baada ya kuchaguliwa kwake angekuwa anakula bata  tu na vipande vya Kuku huko mjini.

"Uungwana ni kushukuru kwani mmenipa heshima kubwa,na mmeniamini kwa kunipa Kazi kubwa ya kuwatumikia nami niseme nitatembea katika ahadi zangu kwenu."alisema Ulega.

Diwani wa kata ya Pazuo  Juma Magahila,akizungumza katika mkutamo huo wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega.

Magahila aliwaeleza wananchi wake kwamba muda uliopo sasa ni wakufanya Kazi nakudai kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni Kazi tu.

Alisema kuwa wakati uliopo ni wa kufanya kazi na zaidi ni kuchapa Kazi Kwa pamoja Kwa lengo la kujenga kijiji cha Kibesa.

"Umoja ndio unaotakiwa na kama kulikuwa na maneno Maneno na hiyo ilikuwa haiepukiki kwani ulikuwa uchaguzi lakini hivi sasa uchaguzi umekwisha mbele yetu kilichobaki nikuchapaka Kazi."alisema. magahiya

Pia aliwataka watendaji wa Halmashauri wakiongozwa na Ofisa utumishi wa Wilaya hii kusaidia wananchi na si vinginevyo na kudai kuwa huwezi kutaja Mkuranga bila kutaja Kibesa."alisema
Awali akisoma risala mbele ya mbunge wao Mwenyekiti wa kijiji cha Kibesa Hamisi Uningwe  alimweleza mbunge huyo kuwa tangu wapate Uhuru wanakero kubwa ya Barabara.

Pia alisema kuwa tatizo lingine ni ukosefu wa Zahanati kwani akina mama wanatembea umbali mrefu na wakati mwingine akina mama wanafia njia Maji safi,ufinyu wa vyumba Vya madarasa.pamoja na 
Naye Mtendaji wa Kata Pazuo Ame Mnyanga alisema
kijiji cha kibesa kina Kaya 32, wakazi 350, nakuongeza kuwa shule ya msingi iko moja, na kwamba kijiji hicho watu wake ni wakulima.

Mbali na ziara hiyo ya kijiji cha Kibesa,pia mbunge Ulega alifika katika kijiji cha Mbezi Mlungwana na kutoa shukrani zake kwa kuchaguliwa ambapo katika mkutano wake huo alichangia sh. 3.5 Kwa ajili ya kununua Betri ya Solar power.

Aidha ulega aliwahaidi wananchi  hao kutekeleza yale yote ambayo aliyahaidi ikiwamo kushughulikia upatikani wa Maji ambayo Kwa kiasi kikubwa imekuwa kero .

Akizungumza kwaniaba ya wenzake Kaim Mketo alimlilia mbunge juu ya upatikanaji wa Maji huku wakijenga hofu ya kusafiri Kutoka Mbezi Mlungwana hadi kijiji cha Nyekenge Kwa ajili ya kufuata Maji.

"Kwakweli tunapata shida mno tunaomba mtusaidie tunateseka Maji hakuna, barabara hakuna kila kitu shida chonde "alisema Mketo.

No comments: