Mkuu
wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis akizungumza na wageni
raia wa Afrika Kusini wanaopanada Mlima Kilimanjaro kwa lengo la
kuchangisha fedha za kununua taulo za watoto wa kike wawapo katika siku
zao za Hedhi.
Mkuu
wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis akimsaidia mmoja wa
wageni hao kubadili lugha ya kiswahili katika simu yake kwenda ya
Kiingereza.
Wageni wakipiga Selfie kabla ya kuanza safari yakuelekea lango la Marangu kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro.
Raia
wa Afrika Kusini wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha
fedha za kunua taulo za watoto wa kike pamoja na kusherehekea kumbukumbu
ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela.
Baadhi
ya wapagazi katika Mlima Kilimanjaro wakishusha mabegi ya wageni hao
kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wageni wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mkuu
wa Vodacom Kanda ya Kaskazini akizungumza na mmoja wa viongozi wa
wageni hao ,Gerry Elsdon kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima
Kilimanjaro.
Wageni
kutoka Afrika Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Vodacom
Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis muda mchache kabla ya kuanza
kupanda mlima Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,Kanda ya Kaskazini.
KAMPUNI
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imedhamini safari
ya siku sita kwa raia 36 wa Afrika Kusini wakiwemo wafanyakazi wa
kampuni hiyo, kupanda Mlima Kilimanjaro yenye lengo la kuchangisha pesa
kwa ajili ya Taulo za watoto wa kike.
Kampuni
ya Vodacom inadhamini safari hiyo ambayo hufanyika kila mwaka kama
sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa Taifa la Afrika Kusini,
Hayati Nelson Mandela, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa Vodacom
kufanya hivyo.
Akizungumza
wakati wa kuanza changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kundi hilo
la watu 36,Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini, Henry Tsamburakis
alisema Vodacom imetoa mawasiliano wakati wote wa safari ya kupanda
mlima ili wasipate tatizo la kushindwa kuwasiliana na ndugu zao pamoja
na kutuma picha za matukio wawapo mlimani.
"Vodacom
Tanzania tunajivunia kuweza kuwadhamini watalii na baadhi ya
wafanyakazi wa Vodacom kutoka Afrika ya kusini kwa mwaka wa pili
mfululizo kwa kudhamini Mfuko wa Mandela ambapo kila mwaka watalii hawa
huja nchini mwetu mwezi wa saba kupanda mlima wa Kilimanjaro wakiwa na
lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike" alisema
Tsamburakis.
"Kwa
upande wetu Vodacom Tanzania tumeamua kuwapatia udhamini wa mawasiliano
ili wasipate matatizo ya mawasiliano wakiwa katika harakati za kupanda
mlima Kilimanjaro waweze kutuma picha au kuwasiliana na ndugu zao kwa
urahisi zaidi kupitia 4G yetu,"aliongeza Tsamburakis.
Alisema
Vodacom imetoa vifaa maalumu (Routers) sita zikiwa zimeunganishiwa
katika mtandao wa kasi huku zikiwa zimewekewa bando ya GB 10
watakazoweza kutumia kwa muda wote watakapokuwa mlimani.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake, Gerry Elsdon ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa
kuwezesha mawasiliano hatua itakayochangia safari yao ya kuelekea katika
kelele cha Uhuru katika mlima Kilimanjaro kuwa rahisi zaidi.
"Niishukuru
kampuni ya Vodacom kwa niaba ya wenzangu, imewezesha mawasiliano yetu
kuwa rahisi sasa,kwa sababu tuliamini kuwa tutakua nje ya mawasiliano
kwa zaidi ya siku sita kumbe sasa tutaendelea kuwasiliana na ndugu na
jamaa" alisema Elsdon.
Kwa
upande wake mratibu wa safari hiyo ambayo hujulikana kama
Treck4mandela,Richard Mabaso alisema lengo la safari hiyo ni kuendelea
kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua Taulo za kike kwa watoto wa kike
wasio na uwezo ili kukitumia pindi wawapo katika siku za hedhi.
""Tunatambua
changamoto zinazowakabili watoto wa kike hasa wale walioko mashuleni
pindi wanapoingia katika siku zao,kupitia Mfuko wa Mandela tumeendelea
kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia angalau kupata Taulo ili waweze
kuendelea na masomo bila ya kuwa na kikwazo." alisema Mabaso.
Alisema
mbali na zoezi hilo kulenga kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa
kike pia limekua likitumika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba
wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela.
No comments:
Post a Comment