Thursday, July 21, 2016

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA NNE KATIKA KATIKA RIPOTI YA MATUMIZI YA FEDHA YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TANZANIA imeshika nafasi ya nne katika ripoti ya utafiti wa matumizi ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kukosa sera ya uratibu fedha kutoka ngazi ya juu hadi chini.

Akizungumza leo na wadau wa mabadiliko ya Tabianchi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga amesema kuwa kama hakuna nia ya dhati kuwa na sera ya matumizi ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi Tanzania itaendelea kuwa nafasi hiyo.

Amesema kuwa nchi ya Rwanda ndio imeshika nafasi ya kwanza kutokana na kuweka sera nzuri katika uratibu na ufatiliaji wa matumizi ya fedha kutoka ngazi ya juu hadi chini.

Mwanga amesema nchi ya Burundi ndio imekuwa ya mwisho katika ripoti hiyo ambapo kutokana na Tanzania na Burundi zinahitaji kuwa na mkazo wa kuwa na sera ya matumizi ili kuweza nchi zinazofadhili zisiwe kuacha.

 Aidha amesema nchi ya Uganda ndio inamfumo mzuri kutokana na kuwa na kituoa cha taarifa ya fedha za matumizi ya mabadiliko ya tabianchi.

Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thabit Jacob,amesema kuwa kunahitajika elimu zaidi katika maeneo ya vijijini juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Amesema Tanzania ikiweka mkakati wa kuwa na sera ya matumizi ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi tunaweza kuondoka na nafasi kutokana na kuwa na sera vitu vingi na vimeweza kufanikiwa.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga akizungumza na wadau wa mabadiliko ya Tabia ya nchi jijini Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wadau wa Mabadiliko ya Tabia ya nchi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi jijini Dar es Salaam leo.
 Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma, Thabit Jacob akifafanua jambo  kwa wadau wa kupambana na mabadiliko ya Tabia ya Nnchi jijini Dar es Salaam leo.
 Mwananfunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es Salaam anayejitolea katika maswala ya mabadiliko ya Tabia ya nchi akitoa maada  kwenye mkutano wa wadau wa mabadiliko ya Tabia ya nchi jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga  akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mabadiliko ya Tabia ya nchi jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments: