Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon
Mwakifamba,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam,leo kuhusu
kuipongeza serikali kupitia wizara husika katika kuanzisha oparesheni ya
kuwakamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini. Kushoto ni Mwenyekiti
wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini,Moses Mwanyilu.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini,Moses Mwanyilu,akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano huo wa kwanza kulia ni Rais wa
Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon
Mwakifamba.
|
Waandishi wa habari wakimsikiliza
mwenyekiti wa chama cha wasambaji wa filamu nchini,Moses Mwanyilu
(hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu wizi wa ulanguzi wa kazi
za wasanii nchini.
Katibu
wa Chama cha Wasambaji wa Filamu Tanzania,Suleiman Ling'ande wa
katikati,akizungumza katika mkutano huo wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti
wa Chama cha Wasambaza filamu Bw. Moses Mwanyilu.
Muigizaji wa Filamu za Bongo Movie
nchini,Kulwa Kikumba Al maarufu Dude wa pili kushoto ,akitoa ufafanuzi katika mkutano huo
juu ya athari za uharamia wa kazi za wasanii mbele ya waandishi wa habari.
Muanzilishi wa Mtandao wa Filamu Central,Myovela Mfwaisa,akiuliza swali katika mkutano huo.
Habari/Picha Na Ally Daud-Maelezo
CHAMA cha Wasambazaji wa Filamu Tanzania na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) vimepongeza
hatua iliyochukuliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia
waziri wake,Nape Nnauye katika kuhakikisha wanatokomeza waharamia na uuzaji wa
kazi za wasanii bila kufuata utaratibu za kisheria zilizowekwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa
chama cha wasambazaji wa filamu nchini,Moses Mwanyilu,alisema kuwa hatua ya
serikali imekuja katika muda muafaka kufuatia kilio cha muda mrefu kutokana na
baadhi ya wafanyabiashara na wasambaji wa filamu na muziki kutoka nje ya nchi wamekuwa
wakiingiza na kuuza bidhaa hizo bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kulipa kodi.
Amesema kuwa wafanyabiashara hao pia wamekuwa
wakidurufu filamu za ndani ya nchi na kuziingiza sokoni bila ya wasanii
kunifaika na kazi zao ikiwemo kazi hizo kutolipiwa kodi hivyo kupelekea kuziuza
kwa bei ya chini ukilinganisha na filamu hapa nchini jambo ambalo linasababisha
soko la filamu za ndani kudidimia.
Aidha Mwanyilu ameongeza kuwa baada ya kilio cha muda mrefu hatimaye
wameona jitihada za serikali kupitia kwa wizara inayohusika na masuala ya sanaa
kuanza kuchukua hatua za makusudi kufanya oparesheni ya nguvu ya kukamata
walanguzi wa kazi za wasanii nchini katika maeneo ya kariakoo.
Kwa niaba ya chama cha wasambazaji wa filamu na
shirikisho la filamu Tanzania na vyama vyote vya shirikisho wanapenda kutoa
shukrani za dhati kwa wizara ya habari kupitia waziri wake,Nape Nnauye kwa
kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),Bodi ya filamu,Cosota na
Baraza la Sanaa Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kazi za
wasanii nchini zinauzwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na unaotambulika.
Naye Katibu Mkuu wa chama cha Wasambaji wa Filamu
Tanzania,Suleiman Ling’ande alisema kuwa tatizo la uharamia katika kazi za
wasanii nchini ni changamoto ya muda mrefu kufuatia kuwepo na sheria ambayo
imeshindwa kukidhi na kusimamia utaratibu unaofaa hasa katika kuhakikisha kazi
za wasanii zinawanufaisha wasanii pamoja na kuliongezea kipato taifa pamoja na
kulipa kodi.
Pia Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon
Mwakifamba,amesema kuwa anaunga mkono zoezi linaloendelea kwa wadau wa kazi za
wasanii cnhini wakishirikian na serikali katika kuhakikisha wanatokomeza
uharamia wa kazi za wasanii wote nchini ili walau kuwapa motisha ya maisha
mazuri waigizaji hao ili waendelee kutengeneza kazi nzuri za kuelimisha jamii.
No comments:
Post a Comment