Saturday, July 2, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Watu 11 wamekufa kwa kuteketea kwa moto na wengine 46 kujeruhiwa katika ajali mbili za barabarani mkoani Morogoro. https://youtu.be/9pmLqB6uHhY 

SIMU.TV: Mamlaka ya usafiri wa anga nchini TCAA ikishikiana na shikika la ndege la Malaysia imeanza uchunguzi wa bawa la ndege lililokutwa katika kisiwa cha Pemba ili kubaini asili ya bawa hilo. https://youtu.be/02oMuYzF44Y

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini TRA imetoa ufafanuzi juu ya ongezeko la kodi VAT katika gharama za miamala ya fedha na kusema haimhusu mteja bali inahusu makampuni ya simu na mabenki. https://youtu.be/opzNYEZiSio

SIMU.TV: Kutokamilika kwa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi 2 na Kilwa Energy imeelezwa kusababisha kutotumika kwa gesi nyingi inayozalishwa nchini.https://youtu.be/FTTjmjjWaRM

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amesema changamoto za kibiashara zilizopo kwenye ukanda wa jumuiya ya Afrika Mashariki lazima zitatuliwe ili kuwezesha wananchi kunufaika na biashara zao. https://youtu.be/OghTTdQhulc

SIMU.TV: Jaji mkuu wa Tanzania Othumani Chande ametoa wito kwa mawakili wapya walioapishwa leo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria za nchi.https://youtu.be/v4mauBgVIoA

SIMU.TV: Washikiriki kutoka asasi za kiraia wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuwaelimisha wananchi kuhusu ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali CAG.https://youtu.be/CiELd6JhxRI

SIMU.TV: Wajumbe wa baraza la wawakilishi wametakiwa kuendelea kuwahamasisha wananchi wao kuendelea kujiunga na mfuko wa bima ya afya. https://youtu.be/-Je2pnMQ9Q0

SIMU.TV: Idadi ya mikopo nafuu ya kuwaendeleza wajasiriamali wadogo nchini inayotolewa na  mamlaka ya usimamizi wa viwanda vidogo SIDO imefikia bilioni 3.6.https://youtu.be/T-xW4BL9sh8

SIMU.TV: Kampuni  ya mawasiliano ya Vodacom imepeleka huduma ya mawasiliano ya mtandao ya bila kuunganisha yaani router kwenye maonesho ya sabasaba.https://youtu.be/r26itV6EzZ8

SIMU.TV: Mamlaka ya ufundi stadi nchini VETA imeongeza idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa kwa mwaka kwenye kozi za muda mrefu na muda mfupi. https://youtu.be/-d7Qf-gbyTw

SIMU.TV: Benki ya NMB imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuisadia jamii ya watanzania katika huduma mbalimbali za kijamii. https://youtu.be/yGQwU7U9GGs

SIMU.TV: Klabu ya Simba imewatambulisha kocha mkuu wa klabu hiyo pamoja na katibu mkuu walioanza kazi leo ili kuiongoza Simba msimu ujao.https://youtu.be/OaM4EdJA2WE

SIMU.TV: Baada ya TFF kusema kuwa wanasubiri taarifa ya CAF kuhusu mchezo wa Yanga dhidi ya Tp Mazembe klabu ya Yanga imesema inashangazwa na jambo hilo maana mchezo huo ulifanyika kwa utulivu. https://youtu.be/J0NE5wT6v3A

SIMU.TV: Japo timu ya Ureno kuonekana kushinda kwa kusuasua katika michuano ya EURO inayofanyika huko nchini Ufaransa lakini imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Poland kwa mikwaju ya penati. https://youtu.be/JbeRIJh2YUI

SIMU.TV: Malawi imemfuta kazi kocha wa timu ya taifa baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo kufuzu kucheza kombe la mataifa ya kombe la mataifa Afrika.https://youtu.be/lpG7rwouO9c

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini TRA imezitaka taasisi za kifedha nchini zikiwemo benki kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu mkanganyiko uliojitokeza juu ya uhalali wa VAT; https://youtu.be/Z7L8uTqFLrk

SIMU.TV: Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini TPA imekabidhi hundi ya shilingi milioni 250 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuchangia utengenezaji wa madawati; https://youtu.be/VYyRtLX5cXg

SIMU.TV: Waumini wa dini ya Kiislam nchini leo wamefanya matembezi ya amani ya QUDS kuadhimisha mateso ya waislam wenzao nchini Pakistan; https://youtu.be/vx88yzwkt4Y

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Namupa mkoani Lindi wameilalamikia serikali yao kwa kuteleza barabara yao kwa muda mrefu sasa; https://youtu.be/mg3Cgt2LnlQ

SIMU.TV: Kampuni ya simu ya Vodacom inaendelea na maboresho ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatoa simu bora ili kuhakikisha watanzania wote wanapata mawasiliano bora; https://youtu.be/xahs-xNgFCo   

SIMU.TV: Rais wa Rwanda Paul Kagame amefungua rasmi maonesho ya 40 ya kibiashara katika viwanja vya kimataifa vya biashara vya mwalimu Julius Nyerere maarufu Sabasaba;https://youtu.be/798dD_hY2u8

SIMU.TV: Shirika la maendeleo ya petroli nchini TPDC limeshauriwa kutafuta masoko zaidi ya kuuza gesi yake badala ya kutegemea wateja wa ndani pekee;https://youtu.be/0ZxYKQSUHA0

SIMU.TV: Shirika la viwango nchini Tanzania TBS limekamata shehena ya vilainishi vilivyochini ya ubora vikiwa sokoni eneo la Kariakoo; https://youtu.be/IOpA-rstl2E

SIMU.TV: Wakulima wa zao la mpunga katika halmashauri ya Mbalali mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwasaidia mikopo yenye riba nafuu; https://youtu.be/Ns9bCQOsdE8

SIMU.TV: Kocha Mcameroon, Joseph Omog ametambulishwa rasmi katika makao makuu ya klabu ya Simba na kusaini mkataba wa miaka 2 kuifundisha klabu hiyo;https://youtu.be/cTjzlEm6sgo

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana Serengeti boys Bakari Shime amesema hatarajii kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kitakachoanza kesho kuvaana na Shelisheli; https://youtu.be/q-VyiZUX4DY

SIMU.TV: Mwenyekiti cha soka mkoa wa Mara Michael Wambura, ameelezea mikakati yake ya kuurudisha mkoa huo katika ramani ya soka baada ya kupotea kwa muda mrefu;https://youtu.be/cA8LRhwGEWI

SIMU.TV: Wanariadha kutoka nchini Kenya, Rudisha na Kemboi wamefuzu mchujo wa kushiriki michuano hiyo itakayofanyika mwezi August  mwaka huu nchini Brazil;https://youtu.be/JfJUXItkhSU

No comments: