Sunday, July 17, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Serikali imetoa muongozo utakaosaidia kuepusha kuendelea kutokea kwa majanga ya moto mashuleni na sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi;https://youtu.be/G9tNYUmjbdk

SIMU.TV: Waziri wa kilimo ufugaji na uvuvi Dr Charles Tizeba ameitaka serikali ya mkoa wa Simiyu kushirikiana na wadau za pamba kuunda azimio litakalosaidia kufutwa kwa mfuko wa pamba; https://youtu.be/X7h5Oa0BJdY

SIMU.TV: Wakazi wa mji wa Nanyamba mkoani Mtwara, wamelalamikia tatizo la ukosefu wa maji kwa muda mrefu sababu inayopelekea kutumia maji machafu yasiyo salama;https://youtu.be/vQAuRdwPHswB

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Makongo juu jijini Dar Es salaam, wamelalamikia tatizo la barabara linahatarisha afya na maisha ya wakazi wa kata hiyo;https://youtu.be/ywUftqR9jfU

SIMU.TV: Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda, amesema wananchi mkoani Katavi wako tayari kufufua viwanda vilivyokufa endapo tu watapelekewa umeme wa uhakika;https://youtu.be/JTC9qkazazY

SIMU.TV: Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, umewaondoa walengwa zaidi ya 26000 kwa kukosa vigezo vinavyowawezesha kunufaika na mradi huo;https://youtu.be/mEQx5MhriJI

SIMU.TV: Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Anastazia Wambura amewataka waandishi wa habari kuelimisha jamii licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa; https://youtu.be/WmyfQbNctAc

SIMU.TV: Serikali Mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa uwanja wa ndege mkoani humo ili kukuvutia maendeleo na uwekezaji  mkoani humo;https://youtu.be/vdQEwdKX2VQ

SIMU.TV: Licha ya Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo kuyafungia maduka zaidi ya 40 yanayojihusisha na uuzaji wa CD feki, bado CD hizo zimezidi kuzagaa mitaani huku zikiwa na stika za TRA; https://youtu.be/OHxK5Fw-SK0

SIMU.TV: Baada ya klabu ya Yanga kushindwa kutamba hapo jana dhidi ya Medeama, wachambuzi wa michezo nchini wameipa nafasi finyu Yanga kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo la shirikisho barani Afrika; https://youtu.be/LIcQMYTkl5s

SIMU.TV: Mchezo wa wavu kwa wanaume na wanawake katika mashindano ya mkoa wa Dar Es salaam, sasa umefikia hatua ya Fainali kwenye viwanja vya ndani vya uwanja wa Taifa; https://youtu.be/KT9l-CuDKMs

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema baada ya kukamilisha zoezi la utengenezaji wa madawati sasa nguvu hiyo inatakiwa kuelekezwa katika ujenzi wa madarasa. https://youtu.be/VEq-I5WLTjs

SIMU.TV: Chama cha watu wenye Ualbino nchini kimeeleza kufarijika baada ya serikali kutangaza adhabu kali kwa watu wanaojihusisha na mauwaji ya watu wenye ualbino.https://youtu.be/3A0vIll0Jm0

SIMU.TV: Wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari Nuru iliopo katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wameazimiana kulipa shilingi elfu 50 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi. https://youtu.be/uP2ieSI_EPo

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Happi amesema kutokana na kukithiri kwa biashara haramu ya ngono eneo la Manzese uwanja wa fisi serikali itafanya tathimini ya eneo hilo na kuwalipa wamiliki wa nyumba ili eneo hilo lipewe mwekezaji.https://youtu.be/WUm2kIXR2yQ

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya amewashauri wakulima wa zao la kakao kuwekea kipaumbele katika uzalishaji wa kakao zenye ubora na kuwauzia makampuni yanayojali jamii. https://youtu.be/4Qtw_IIMxOc

SIMU.TV: Baadhi ya  waumini mkoani Morogoro wakishirikiana na kiongozi wao nabii Joshua wameamua kutoa elimu juu ya  ugonjwa wa kipindupindu kwa kutumia jeneza.https://youtu.be/XdJ5oKwSSSE

SIMU.TV: Naibu waziri TAMISEMI Seleman Jafo ametoa wito kwa madaktari na wauguzi wa hospitali ya Kisarawe kuzingatia weledi wa kazi na kutowaudhi wagonjwa.https://youtu.be/u14pfaM1Lq8

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Kilungule jijini Dar es Salaam wameanza harakati za ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo ili kusogeza huduma za afya karibu. https://youtu.be/w-6oGST4eLc

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa amewataka wakandarasi wanojenga barabara ya Mankanka hadi Mtambaswala mkoani  Mtwara kujenga barabara hiyo kwa kiwango kinachotakiwa.https://youtu.be/aRHxFIA6thU

SIMU.TV: Taasisi ya madam Sofy Charity imetoa msaada kwa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi katika hospitali ya taifa Muhimbili. https://youtu.be/p-f4Ff50nYE

SIMU.TV: Kufuatia sare ya Yanga na Mediama ya nchini Ghana wadau na washabiki wa soka wameitaka klabu ya Yanga kutofifisha matumaini na kutazama michezo ya mbeleni.https://youtu.be/9V7MiO4IsPs

SIMU.TV: Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuendeleza sanaa nchini diwani wa kata ya Kilungule Said Fella amekisaidi kikundi cha ngoma cha Kilungule Youth Group.https://youtu.be/eWNvdVEbwxQ

SIMU.TV: Baadhi ya maofisa wa TRA wamebainika kutoa stika kwa wauzaji wa CD feki na kukwamisha juhudi za serikali za kupinga wizi wa kazi za wasanii.https://youtu.be/dpB11s7FHj8

SIMU.TV: Naibu waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo amewataka vijana kushiriki mashindano ya baiskeli pale wanapopata nafasi. https://youtu.be/qI-R0k4agTA

SIMU.TV: Timu ya Chelsea imefanikiwa kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Leicester city Ng’olo Kante kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia pound milioni 30.https://youtu.be/w9IjTifHejQ

No comments: