Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India.
Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili.
Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Othmani Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga.
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili.
Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo.
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo.
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
No comments:
Post a Comment