Saturday, July 30, 2016

Mtanzania mkazi wa UK Karrima Carter na wahisani wenzie kutoka Norwich watoa misaada Tanzania



Kundi la watoto yatima wanaotunzwa na Karrima na wahisani wenzake Waingereza kutoka Norwich hapa Uingereza
Baadhi ya wahisani kutoka Norwich wakiwa katika halfa ya utoaji misaada kwa kituo cha kulea yatima, Bagamoyo


Mwanadada wa Kitanzania, Karrima Carter, mwenye makazi yake Norwich, hapa Uingereza, wiki hii ameshirikiana na wahisani wenzake kutoka Uingereza kutoa misaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima huko Bagamoyo na uzinduzi wa vyoo vilivyokarabatiwa kwa uhisani wa dada huyo na wahisani wenzake kutoka Uingereza.


Tukio la kwanza lilifanyika Jumapili iliyopita na kuhudhuriwa na baadhi ya wasanii mbalimbali kama vile Gabo na Faiza Ally (ambao walialikwa rasmi kwa minajili ya kuwapa tabasamu watoto yatima), na tukio la pili lilifanyika Jumatatu iliyopita.

Picha na maelezo ya tukio la tatu la kukabidhi madawati zitawajia kesho. Awali, Karrima alisita kuhusu wazo la ku-blogu kuhusu matukio haya akisema kwamba asingependa 'publicity' lakini mie binafsi nilimshauri kuwa kuweka hadharani habari hizi kunaweza kusaidia kuwahamasisha Watanzania kuhusu utamaduni wa kutoa misaada kwa wenzetu wenye uhitaji, eneo ambalo ni maarufu hapa Uingereza lakini ni geni kwa nchi nyingi za Afrika.

Karrima amekuwa akijibidiisha katika sekta hiyo ya misaada kwa wenye uhitaji kwa kitambo sasa. na amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kwa wakazi wenzie wa Norwich.

Karrima n wahisani wenzake kutoka Norwich, uingereza, mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa hafla mbalimbali za utoaji misaada

Hafla ya kuzindua vyoo katika Shule ya Msingi Ilala, ambavyo vilifanyiwa ukarabati kwa uhisani wa Karrima na wenzie kutoka Norwich, Uingereza

Karrima na wahisani wenzie kutoka Norwich wakiwa shuleni Ilala
Mmoja wa wahisani kutoka Norwich akisaini kitabu cha wageni
Karrima akisalimiana na mmoja wa wadau
Karrima akisalimiana na walimu
Moja ya vyoo vilivyofanyiwa ukarabati
Ukitoa 'viboko' na ugumu wa masomo, moja ya vitu vinavyowafanya wanafunzi wengi wachukie shule, hasa za msingi, ni vyoo visivyofaa kwa matumizi ya binadamu. Bila shaka jitihada hizi za Karrima zitahamasisha Watanzania wengi zaidi kujitokeza katika ufadhili wa taasisi zetu.

Hafla ya utoaji misaada kwa kituo cha kulea yatima huo Bagamoyo
Karrima, Gabo, Faiza na mmoja wa wahusika wa kituo cha kulea yatima Bagamoyo

Faiza, mmoja wa walioshiriki katika maandalizi ya hafla hiyo huko Bagamoyo
Msanii maarufu wa Bongo Movies, Gabo, naye allijumuika katika hafla hiyo. Pembeni yake ni mmoja wa wahisani kutoka Norwich.
Gabo akiwaburudisha watoto yatima
Karimma akitoa hutuba katika hafla hiyo
Nathani Mpangala, mmoja wa walioshiriki katika maandalizi ya hafla hiyo
Mmoja wa wahisani kutoka Norwich akijiandaa kupata msosi

No comments: