Monday, July 4, 2016


Mkufunzi klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji chipukizi jinsi gani ya kuanza kuogelea kwa staili ya backstroke.
Waogeleaji chipukizi chini ya miaka minne wakishiriki katika mafunzo hayo kwa vitendo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya DIA yaliyoandaliwa na klabu ya Dar Swim Club chini ya ukufunzi kutoka klabu bingwa ya mchezo huo nchini Dubai, Hamilton Aquatics.
Mkufunzi wa klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji chipukizi jinsi gani ya kuelea ndani ya maji kwa staili ya backstroke.
Waogeleaji Adam Kitururu na Celina Itatiro wakifanya mazoezi baada ya kupatiwa mafunzo ya kuogelea kwa staili ya backstroke huku wakiwa na glasi katika paji lao la uso. Lengo lakufanya hivyo ni kuogelea kwa kufuata masharti ya staili hiyo.
Kocha Nebojsa Durkin (wa pili kulia) akiwaelekeza makocha wa Dar Swim Club mbinu mbalimbali za kisasa za kuogelea .
Kocha Katy Morris akiwasimamia waogeaji chipukizi (watoto) jinsi gani ya kuelea kwenye maji na kuongelea kwa freestyle na backstrokeWakufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea wa klabu bingwa ya Mashariki ya Kati (Middle East) ijulikanayo kwa jina la Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin ma Katy Morris wamesema kuwa Tanzania inaweza kupata sifa kubwa katika michezo duniani kupitia mchezo wa kuogelea.

Wakufunzi hao walisema hayo katika semina inayoendelea ya mchezo huo kwa waogeleaji na makocha wa klabu marufu ya Dar Swim Club (DSC).Durkin alisema kuwa amefuraishwa na vipaji vya mchezo huo kutoka kwa waogeleaji wa DSC na anaamini kuwa siku moja, Tanzania itatoa bingwa wa dunia kupitia mchezo huo.

“Nimefurahi kuona kuwa mchezo una mwamko sana na wachezaji wanaupenda, pia Tanzania ina makocha wazuri wenye elimu ya kutosha, naamini kama juhudi hizi zitaendelezwa, nchi itapata wawakilishi wazuri katika mashindano ya kimataifa na kuweza hata kutwaa ubingwa wa Dunia,” alisema Durkin ambaye ni raia wa Serbia.Alifafanua kuwa amefuraishwa na waogoeleaji chipukizi ambao umri wao ni chini ya miaka minne.

“Nimevutiwa kuona hata Tanzania hasa klabu ya DSC ina waogeleaji watoto ambao wanaupenda mchezo, hii imenivutia sana, hapa utapata wachezaji ambao wataupendea mchezo kuanzia utotoni na huu ndiyo mwamko ambao utaleta matunda katika mchezo,” alisema.Kwa upande wake, Katy ambaye ni mwanadada alisema kuwa wadau wa mchezo huo wanatakiwa kusaidia kufikia malengo hayo kwani bila uwekezaji mkubwa, bado mchezo utakuwa chini kutokana na ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kisasa.

Katy alisema kuwa DSC imeonyesha nia ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa na kuomba wadau waunge mkoni. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na kampuni za Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom.
Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro amesema kuwa lengo lao ni kuona Tanzania inafanya vizuri katika mchezo huo kimataifa. Alisema kuwa DSC imeamua kupambana katika kuleta maendeleo ya mchezo wa kuogelea hapa nchini.

“Tunahitaji sapoti katika mchezo huu, lengo ni kuona waogeleaji wanapata maendeleo makubwa kwa kufikia viwango, nawaopongeza wadhamini Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom kwa kutuunga mkono, gharama za kuwaleta walimu kutoka nje ni kubwa sana,” alisema Inviolata. 

No comments: