Thursday, July 14, 2016

Mjue Kiundani 'Simba wa Afrika' Robert Mugabe

Na Geofrey Chambua
1. Mzaliwa wa Februari 21. 1924; Komredi Robert Gabriel Mugabe Ni mtoto pekee aliyesalia katika familia yao kwani kaka zake wawili walifariki akingali mdogo sana na baba yake alitelekeza familia yao mnamo mwaka 1934 na kumlazimu mama yake kuolewa na mwanaume mwingine. Ingawa unamjua Mugabe kama Rais wa Zimbabwe ukweli ni kwamba Baba yake mzazi Gabriel Matibili ni Mmalawi aliyekua fundi seremala ila mama yake ambaye ndiye aliyemlea ni Mshona wa Zimbabwe kwa asili. 

2. Kwa miaka 92 amekua​ akitumia zaidi vyakula vya asili ya mimea (Vegetarian) chakula chake kikuu ikiwa ni maboga ingawa aghalabu hula nyama pori na hasa nyama ya ​S​imba na ​T​embo. Mugabe pia hatumii kileo wala kuvuta sigara

3. Huamka saa kumi alfajiri kila siku kwa mazoezi mepesi na hupenda sana kusikiliza BBC baada ya hapo, huenda hii ikaelezea kwa nini husinzia sana hata kwenye hadhara
4. Ana jumla ya shahada SABA. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika ​C​huo ​K​ikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine sita kwa njia ya masafa (Distance Learning) kati ya hizo mbili ​za Sheria ​akiwa gerezani. Kazi yake ya kwanza kabla ya kujiunga na siasa ni UALIMU na alianza kufundisha Chuo cha Ualimu Chalimbana nchini Northen Rhodesia (Zambia kwa sasa) kisha Apowa Sekondary nchini Ghana. Mugabe amekua akisisitiza sana katika elimu nchini mwake na ameiwezesha Zimbabwe kuweka rekodi ya juu ya kufuta ujinga Afrika kwa 90%. Mnamo Mwaka 2005 alitunukiwa shahada ya heshima ya Uprofesa na Chuo Kikuu cha Diplomasia huko China kwa uwezo wake wa kusomea karibu fani zote muhimu duniani ikiwemo sheria, uchumi, historia, sayansi, sanaa, utawala na elimu.......yasemekeana rafiki mkubwa wa maisha ya Mugabe ​tangu utotoni ​ ​​ni 'Kitabu kwa sana'​ ​ 

5. ​Upande wa michezo, ​Hupendelea sana Kriketi na Kisoka yeye ni mnazi wa Chelsea ya Uingereza na Barcelona kwa Upande wa Spain na yasemekana ana mizuka sanaya kisoka pia ...... 'Huwa nina midadi sana ninapotazama kandanda, 'wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwa kupiga mateke chochote kilicho mbele yangu”

6. Mugabe pia ni mcheza kamari maarufu (kubeti) ingawa kisiri sana kwani mwaka 2000 alistua wengi aliposhinda ZimDola 100,000 kwenye Bahati Nasibu iliyoendeshwa na Benki ya Biashara (ZimBank)
7. Mtoto wake wa tatu alimpata mwaka 1997 wakati huo Bob akiwa na miaka 73 alizaa na aliyekua karani muhtasi wake aitwaye Grace Marufu (miaka 38) ambaye kwa wakati huo alikua mke wa mtu (mchepuko) na akalazimika kumtaifisha kama mkewe wa TATU katika maisha yake ya ndoa

8. Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-Bob haamini sana katika ufuasi wa dini. Alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, Jongwe huyu wa Afrika alikiri kwamba hata maswahiba wake wengi humchukulia Mugabe kama mpagani tu kutokana na mtindo wa maisha yake (life style)​.

9. Tayari ameshaweka wazi nia yake ya kuwania kiti cha Uraisi mnamo mwaka 2018 ​ambapo ​panapo majaliwa atakua na miaka 94 hivyo atakua ametimiza miaka 30 ya uraisi iliyotanguliwa na miaka 7 ya Uwaziri Mkuu (The oldest and longest serving President in the whole world)
Al​iwahi kuulizwa n​a waandishi wa habari 

​Mwandishi: Mr President, When will you say goodbye to the people of Zimbabwe? (Lini utawaambia kwa heri wananchi wa Zimbabwe?)

Mugabe: Where are they going? (Kwani wanaenda wapi?)​
10. Mugabe ambaye hujulikana sana kwa majibu na misemo yenye utata sana hasa kwa waandishi wa habari, amewahi kuingia kwenye kinyang'anyiro cha wateule wachache wa kuwania tuzo ya amani ya Nobel ingawa hakushinda kufuatia mfululizo wa mauaji nchini kwake kipindi hicho baada ya kumtimua Joshua Nkomo kutoka Baraza lake la ​Ma​waziri hali iliyowachukiza Wandebele na kuzua mapigano ya kimbari dhidi ya Washona.
11. Mugabe amejipatia umaarufu Barani Afrika na Kwingineko Duniani kwa misimamo yake thabiti kiasi cha kuitwa dikteta wa aina yake (In 2007, Parade magazine ranked Mugabe the 7th worst dictator in the world) na hasa kupinga ukoloni mamboleo nchini mwake na pia tabia za kushiriki mapenzi ya jinsi moja ambapo mnamo mwaka 1997 Maha​ka​ma​ ​ya nchi hiyo ilimtia hatiani kwa makosa 11 mtangulizi wake Cannan Banana kwa kushiriki ngono kinyume cha maumbile (sodomy). Banana ndiye Rais wa Kwanza wa Zimbabwe.


12. Mnamo mwaka 1975, Mugabe alichaguliwa kuwa Rais wa ZANU-PF huku akingali anatumikia kifungo kwa chagizo kubwa la Askofu Abel Muzorewa 

Mugabe ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani baada ya kutimia umri wa miaka 92 mwaka huu na tayari Chuo kimoja cha utafiti nchini Uingereza kimetaarifu Mugabe kuishi milele kutokana na mwili wake kuwa na vinasaba ambavyo havina urafiki na mauti licha ya kuzushiwa kifo mara kadhaa. 
Mnamo Februari 16 mwaka huu alinukuliwa akisema kwamba hana mpango wa kustaafu URAIS hadi 'Mwenyezi Mungu atakapomuita' 

Mwandishi: Mweshimiwa Rais, huoni kwa umri wako wa miaka 89 ni wakati mwafaka wa kupumzika na kuachana na kazi?

Mugabe: Umewahi kujaribu kumwuliza swali hili Malkia Elizabeth au swali lako ni kwa ajili ya viongozi wa Kiafrika tu?

No comments: