Thursday, July 28, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA MKURANGA, ABDALLAH ULEGA AENDELEA NA ZIARA YAKE KUWASHUKURU WANANCHI.

 Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Nyakenge,kata ya mkamba ikiwa ni sehemu ya utaratibu ambao ameuweka wa kwenda kushukuru,na kuhimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo leo   mkoani Pwani.
 Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akisisitiza jambo mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauli ya Wilaya ya Mkuranga Juma Abed katika mkutano wa Mbunge huyo wa kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Tungi kwakumchanguwa kama Mbunge wa jimbo hilo mwaka jana.
 Wajumbe wa bodi ya chama cha msingi cha ushiriki wa Korosho wakimsikiliza Mbunge wajimbo hilo Abdallah Ulega ambapo alifika katika kijiji cha kizapala kilichopo kata ya Mkamba kwa lengo la kukaguagodauni la kuhifadhia Korosho,amapo pia katika kikao hicho alichangia Zaidi ya sh. Laki sita.
 Mtendaji wa kijiji cha Tungi kata ya Mkamba Idd Kambangwa mbaye pia ametumbuliwa jipu kutokana na utendaji wake mbovu akikabidhi risala  kwa Mbunge Abdallah Ulega mara baada ya kufanya ziara ya kushukuru kijijini hapo leo.
 Wananchi wa kijiji cha Tungi, kata ya Mkamba wilayani Mkuranga wakimsikiliza kwa makini Mbunge wao Abdallah Ulega wakati akitoa salamu zake za kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanyika mwakajana ambapo pia katika mkutano huo Ulega alichangia sh. Milion moja kwa ajili yakuaza ujenzi wa shule msingi kijijini hapo.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa kijiji cha Tungi kata ya Mkamba mara baada ya kuwasili kijiji hapo kwa lengo la kuwashukuru kwakufanikisha kumchagua kuwa Mbunge wao katika uchaguzi uliofanyika 2015.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments: