Sunday, July 3, 2016

MA- DC WATANO WAPYA WA MKOA WA LINDI WALA KIAPO

 Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wa wilaya tano za mkoa huo pamoja na watendaji wa ofisi yake baada ya kiapo

 Mmoja wa Wakuu wa wilaya akila  kiapo


Na Mathias Canal, Lindi 
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo huku kila mmoja akiahidi utendaji uliotukuka katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi husika.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo mkuu huyo amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati linazaa taswira chanya kwa kuhakikisha madawati yanatimia kama ambavyo agizo la rais lilitolewa hivi karibuni la kuhakikisha wanafunzi wanaketi katika madawati pasipo kuwa na mbanano.
Wakuu wa Wilaya  walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngumbiagai na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Akhibu Muwango.
RC Zambi amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm ili kukamilisha ahadi zilizoahidiwa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kampeni zilizoanza Agosti na kumalizika Octoba mawaka jana.
Pamoja na hayo mkuu huyo pia amesema kuwa anatarajia kuanzishaTuzo ya Mkuu wa wilaya kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kila kata ambapo Vigezo watakubaliana na kamati hiyo.
Wilaya ya lindi ni moja kati ya wilaya zilizopo mkoani lindi zinazojihusisha zaidi na kilimo kuliko masomo Muwango amesema kuwa atahakikisha anaanzisha kamati ya maendeleo ya Elimu ya wilaya ambapo Kamati hiyo itakuwa na wataalam na watu maarufu wa Wilaya ya Nachingwea na kamati hiyo itajiwekea mikakati ya uboreshaji Elimu, hivyo mkuu wa Wilaya atatashirikiana na wataalamu wa Halmashauri kuona mikakati hiyo inafanikiwa.




No comments: