Sunday, July 3, 2016

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Simu.tv: Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA limesema litaendelea kuwatambua watafiti mbalimbali waliofanikisha kutambua na kugundua vitu mbalimbali kwa wanyama; https://youtu.be/kbnmkrVVa-Q

Simu.tv: Wananchi wa kata ya Gumbiro wilayani Songea mkoani Ruvuma wameulalamikia uongozi wa kata hiyo kwa kuhusika na wizi wa mbao za madawati; https://youtu.be/yWxdxsxTRJ0

Simu.tv: Wakazi wa Chamazi wilayani Temeke mkoani Dar es salaam wamelilalamikia shirika la umeme TANESCO kwa kufikisha taarifa za uongozi kwa Waziri Porf. Muhongo juu ya malipo ya fidia zao;https://youtu.be/n9JIKC1stb0

Simu.tv: Shirika la umeme TANESCO kanda ya Dar es salaam limeendelea kuwasaka wezi wa umeme kwa kujiunganishia umeme kinyume na sheria; https://youtu.be/oJ_IZ4DeVLo

Simu.tv: Kampuni ya simu ya Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya TECNO wamezindua aina mpya ya simu inayoendana na matumizi ya huduma ya 4G; https://youtu.be/z4xFfgNrfhU

Simu.tv: Kuelekea mwishoni mwa mfungo wa mwezi wa ramadhani, waislamu nchini wameombwa kuendeleza umoja na amani katika maisha yao yote; https://youtu.be/OnguWgnONHM

Simu.tv: Timu ya Taifa ya vijana Serengeti boys imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwagaragaza wapinzani wao Shelisheli kwa jumla ya mabao 6-0; https://youtu.be/euHBwXE1V8E

Simu.tv: Kamati ya maadili ya shirikisho la mpira nchini TFF imeagiza sekretarieti ya shirikisho kumuandikia tena barua yenye mashiko msemaji wa klabu ya Yanga baada ya ile ya awali kuwa na dosari nyingi;https://youtu.be/lyf5KNLXql4

Simu.tv: Viongozi wa dini hapa nchini wametakiwa kuwafundisha waumini wao upendo na uzalendo ili kulinda amani ya nchi. https://youtu.be/HJgCtCShp9k

Simu.tv: Viongozi wa baraza kuu la waislamu BAKWATA mkoani Dodoma wamewataka waumini wa kiislamu kutumia siku chache za mfungo zilizobaki kufuturu pamoja na watu wenye mahitaji na watoto yatima.https://youtu.be/MBaM3xxK15k

Simu.tv: Wizara ya kilimo mifugo na uvuvi imesema haitasita kumchukulia hatua afisa ushirika yeyote atakaye bainika kufanya ubadhirifu na kusababisha chama cha ushirika kufa. https://youtu.be/0SwwC-oMRxg

Simu.tv: Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake katika mkoa mpya wa Songwe ambako utapita na kukagua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 9.7. https://youtu.be/eYrEp58wKaQ

Simu.tv: Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema wabunge wa nchi za jumuiya ya madola wanawajibu wa kuzisadia nchi zao katika kubana matumizi. https://youtu.be/LtWeuGi87Q4

Simu.tv: Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ametoa siku tano kwa wakandarasi waliopewa kazi ya kutengeneza madawati kuhakikisha wanamaliza kazi hiyo. https://youtu.be/V29vwfM_QTE

Simu.tv: Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 imefanikiwa kufuzu mzunguko wa pili wa michuano ya kuwania kufuzu fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 barani Afrika. https://youtu.be/fx0c0VGxU3c

Simu.tv: Kamati ya maadili ya TFF imetupilia mbali shauri lilokua linamkabili afisa habari wa klabu ya Yanga kutokana na kukiukwa kwa vifungu vya sheria. https://youtu.be/TCH7PwXmPsU

Simu.tv: Kiungo wa timu ya taifa ya Wales Aron Ramsey amesema anaamini timu yake itaifunga Ureno katika mchezo wa nusu fainali kwenye michuano ya EURO. https://youtu.be/BRaOg89J6DU

Simu.tv: Mabingwa wa dunia timu ya Ujerumani usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya EURO baada ya kuitoa Italia kwa mikwaju ya penati. https://youtu.be/FYm32Y6YjDg

No comments: