Saturday, June 11, 2016

ZAIDI YA BILIONI 23 ZAOKOLEWA KWA KUONDOA WATUMISHI HEWA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairukiakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo hufanyika Juni 16 -23 kila mwaka.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 23 kwa kuondoa watumishi hewa katika mfumo malipo ya mishahara ya serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki  jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana  mara baada ya kuanza kwa kutafuta watumishi hewa wa serikali.

Amesema kuwa watumishi ambao wameshaondolewa tangu Machi, 1 hadi Mai 30 ni watumishi 12,246 ameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ya Serikali kwa sababu mbalimbali ikimo kutimiza umri wa Kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kuhitimishwa kwa mikataba.

Aidha amesema kuwa wasingeondolewa kwenye mfumo wa mishara kwa wafanyakazi wa serikali zaidi ya shilini Bilioni 25 zingepotea.

No comments: