Saturday, June 18, 2016

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO

SIMU.tv: Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu amezindua harambee ya kuchangia bweni la wanachuo wa kike katika chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro. https://youtu.be/FwP2srKVCtw
SIMU.tv: Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi limesema linaunga mkono maamuzi ya rais Magufuli chini ya kauli mbiu ya Hapa kazi tu katika kuwaletea wananchi maendeleo;https://youtu.be/JARk3kroOik 
SIMU.tv: Chama cha waandishi wa habari Mbeya kimeanza rasmi harakati za kuwahamasisha waandishi wa habari kuwa na sifa ya taaluma ya kazi hiyo; https://youtu.be/j4tlEqLC_n0
SIMU.tv: Kampuni ya reli TRL imewalalamikia baadhi ya wananchi waishio karibu na miundombinu ya reli kufumbia macho waharibifu wa miundombinu hiyo. https://youtu.be/3t7G2qu-s-w
SIMU.tv: Sekta ya utalii katika jumuiya ya Afrika inaweza kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi ikiwa nchi husika zitatumia ipasavyo fursa za soko la utalii wa ndani. https://youtu.be/vmCY-EiacCc
SIMU.tv: Fuatilia mazungumzo kuhusu tukio lililompata  hivi karibuni msanii wa zamani wa bongofleva Rehema  Chalamila almaarufu kama Ray C: https://youtu.be/HlpYIJ50Mbc?t= 
SIMU.tv: Timu ya taifa ya Italia yafuzu hatua ya pili ya michuano ya EURO 2016 kwa kuifunga  timu ya taifa ya Sweden kwa jumla ya goli 1-0; https://youtu.be/EnI4uXWpZj0 
SIMU.tv: Naibu waziri wa habari sanaa na michezo apokea msaada wa mageti kwa lengo la kuboresha miundombinu ya vyoo uwanja wa taifa; https://youtu.be/-yPGgfK150M
SIMU.tv: Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF laingilia kati mgogoro uliojitokeza wakati wa uchaguzi wa chama cha soka cha Kinondoni KIFA; https://youtu.be/L1dwAZyYQS4

No comments: