Tuesday, June 21, 2016

WIZARA YA HABARI YAKUTANA NA WADAU WA KUJADILI NA KUBORESHA SERA YA SANAA ZA MAONESHO


Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na wadau wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho kuhusu mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na kulia ni Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Kundi.Na Anitha Jonas – WHUSM Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. William Chitanda akieleza changamoto za shirikisho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Bw. Efraim Zakaria kutoka kikundi cha Watoto Arts Organization (WAAO). 
Katibu wa Kikundi cha Binti Leo Bi. Agness Lukanga (katikati) akieleza utendaji wa kikundi chao kwa watendaji wa masuala ya Sanaa na Utamaduni wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga. 
Mjumbe wa Kikundi cha Sherehe Arts Association (SAA) Bi. Columba Samjela akiwaeleza watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) mikakati waliyonayo ya kuimarisha Sanaa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa (SAA) Bi. Grace Meena.
HAB5

Mjumbe wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. Denis Mango akifafanua shughuli za shirikisho katika kikao kilichofanyika Juni 21,2016 Jijini Dar es Salaam na Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Katikati ni Bw. Omari Kichapwi, Mjumbe wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA). 
Mjumbe wa Kikundi cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) akieleza jambo kwa Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa Sanaa ya Mashairi. Kulia ni Mjumbe wa UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala. 
Baadhi ya wadau wa Sanaa za Maonesho walioshiriki kikao na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Shani Kitogo (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo kuhusu fani ya ushariri leo jijini Dar es Salaam. 
Mjumbe wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga akitoa maoni ya kuboresha sekta ya Sanaa za Maonesho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mjumbe wa UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.

No comments: