Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Geita (GGM), Tenga Tenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu Mgodi wa GGM kupandisha watu 100 Mlima Kilimanjaro na wengine watazunguka mlima wa Kilimanjaro kwa baiskeli kwaajili ya kuchangia fedha za mfuko wa Kili challenge ambao ni mapambano dhidi ya Ukimwi. Katikati ni Balozi wa Kili challenge Msanii, Mrisho Mpoto, Kushoto ni Mwakilishi wa tume ya Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Peter Dickson.
Balozi wa Kili Challenge na msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto akifafanua jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwaajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga.
Julai 16 hadi 22 Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) ukishirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi wanatarajia kuwapandisha katika Kilile cha Mlima wa Kilimanjaro watu 50 na wengine 50 watauzunguka mlima kwa baiskeli ikiwa ni kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Mgodi wa Geita (GGM), Tenga Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Kilimanjaro Challenge kwa mwaka huu litajumuisha watu kutoka nchi mbalimbali.
Amesema kuwa Balozi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita kwa mwaka huu ni Msanii wa nyimbo za Mashahiri, Mrisho Mpoto atakuwa na watu watakaoshiriki wa Kili challenge hadi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Nae Msanii wa nyimbo za Mashahiri, Mrisho Mpoto amesema kuwa watanzania tuunge mkono kwa pamoja katika sehemu kuchangia au kumuelimisha jamii kuhusina na mapambano dhidi ya UKIMWI yalete mabadiliko.
“Mimi kama balozi wa Kili challenge, naamini kwamba jitihada zinazofanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na watanzania wote na wadau wenye machungu na nchi hii” Alisema Mpot. Hebu tuungane kwa pamoja kila mmja wetu katika sehemu yake eitha kwa kuchangia au kumuelimisha mwenzake ili mapambano haya yalete mabadiliko” alisema Balozi Mpoto.
Fedha zinazopatikana katika mfuko huu zinapelekwa katika kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya ushauri nasaha na upimaji wa ukimwi ambapo baadhi yao ni vie vilivyoko Tanga pale Segera, Manyoni na Geita. Kituo cha watoto yatima Moyo wa Huruma na asasi nyingine zaidi ya 30 zimenufaika na mfuko huu.” Alisema mwakilishi wa TACAIDS, Dickson Peter.
No comments:
Post a Comment