Afisa kutoka TTCL, Fredrick Benard (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda la TTCL.
TTCL wakitoa huduma kwa wateja katika maonesho ya Sabasaba
Wafanyakazi wa TTCL wakitoa huduma kwa wateja.
Wafanyakazi wa TTCL wakiwakaribisha wateja katika Banda.
Wateja wakipata maelezo kuhusu huduma za TTCL, katika viwanja vya sabasaba
Wananchi waendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) kununua bidhaa bora za 4G katika viwanja vya Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba.
Akizungumza katika Maonesho hayo, Emerco Mashele Afisa kutoka TTCL amesema kuwa katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya SabaSaba, kampuni imeendelea kuwaletea watanzania bidhaa nzuri za 4G – LTE, zenye kiwango kikubwa cha ubora, bei nafuu na uhakika.
“Safari hii tumewaletea Wananchi bidhaa bora na nzuri katika matumizi ya mawasiliano ya simu. Kwa huduma zetu tunatoa fursa kwa wateja wetu kupata intaneti yenye kasi ya 4G ukiwa na Laini za 4G ambazo zinapatikana hapa katika Banda TTCL na ofisi za TTCL katika jiji la Dar es salaam” amesema Emerco.
Aidha, Bw. Emerco aliongeza kuwa katika Maonesho haya ya SabaSaba, TTCL inatoa fursa ya wananchi kupata laini ya 4G, Modemu ya 4G, Mi-Fi ya 4G na Routers ya 4G.
Katika maonesho haya tuna laini za 4G ambazo zinapatika hapa na katika ofisi zetu za TTCL, Mteja anaweza kifaa cha 4G Mi-Fi ambapo mteja anaweza kuunganisha watu wengine 10 na kupata intaneti katika ubora ule ule. 4G Routers inauwezo wa kuunganisha watu 32 na inauwezo kwenda katika ubora ule ule, Aidha pia Routers inatoa fursa kwa watumiaji kupata huduma simu ya Mezani.
No comments:
Post a Comment