Monday, June 13, 2016

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA WAPONGEZA MRADI WA HUAWEI 'SEEDS FOR THE FUTURE.

Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kumaliza programu ya wiki tatu ya“Seeds for the future” ambayo ilifanyika katika makao makuu ya Huawei Technologies yaliyopo Shenzhen, China. Programu hiyo inaendeshwa na kudhaminiwa na Kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu nchini Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Lt. generali (Mstaafu) Abdulrahaman A. Shimbo katika ufunguzi rasmi wa programu ya “Seeds for the future” ambapo wanafunzi 10 kutoka Tanzania walipata fursa ya kujifunza kwa vitendo juu ya fani hiyo ya teknolojia na mawasiliano kwa muda wa wiki tatu, programu iliyodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Wanafunzi 10 kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea sehemu ya makumbusho katika mji wa Shenzhen nchini China walipokuwa nchini humo kushiriki mafunzo kwa vitendo kupitia programu ya Seeds for the Future” inayoendeshwa na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.

Shenzhen, China. 08 Juni 2016. Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini ambao walikwenda China kuhudhuria mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (TEHAMA), wameipongeza Kampuni ya Huawei Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wenye lengo la kuongeza ufanisi kwenye masuala ya TEHAMA nchini na kuongeza uelewa juu ya katika sekta ya mawasilino na kuhamasiha ushiriki wa kimataifa katika Teknolojia ya habari na mawasiliano.

Wakizungumza wakati wa mahafali baada ya mafunzo ya programu ya Seeds fo the Future" katika makao makuu ya Huawei Shenzhen nchini China, walisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na Huawei ili kuleta maendeleo katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania.

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ahmed Sufiani Makame (22) alisema mafunzo waliyopata yamewawezesha kufahamu teknolojia mpya kabisa ambayo awali hawakuwa nayo na hawakuipata  katika vyuo vya nchini Tanzania, jambo lililowapa changamoto ili kuweza kukabiliana na mabadiliko yaliyopo katika sekta ya ajira watakapoajiriwa hapo baadaye.

"Alisema katika karne hii ya 21 waajiri huhitaji wafanyakazi ambao wanauzoefu wa kutosha na elimu bora. Wanahitaji waajiriwa wao wawe na ujuzi na mtazamo chanya. Ninashukuru sana Huawei kwa kutupa nafasi ya kuvumbua mapya katika ulimwengu wa teknolojia.

Alisema kutokana na mafunzo waliyoyapata nchini China, kwa sasa wamepata ujuzi ambao watautumia kutatua changamoto zilizopo zilizopo kwenye kampuni za mawasilino nchini Tanzania. Aliongeza kuwa, kupitia elimu masafa (e-learning), usalama wa mitandao, mpangilio wa miji, mifumo ya mtandao, 3G, 4g, mifumo ya data serikalini na hospitali ni mojawapo ya  vitu ambavyo vitaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kimaendeleo  katika sekta ya TEHAMA.

"Wakati wa mafunzo yetu China, tuliona ni namna gani Huawei imejipanga na mabadiliko ya kiteknolojia wakiwa na kaulimbiu yao 'ulimwengu uliounganishwa'. Mafunzo tuliyoyapata yametupa mwanga kuzishauri kampuni za mawasiliano pamoja na serikali kuwa wanapaswa waendane na maendeleo ya teknolojia ya kisasa ulimwenguni," alisema.

Alisema  amepata uzoefu  wa mifumo ya 3G NA 4G na mifumo inayotumika kwenye kompyuta na namna ya kuzitengeneza na kuingiza huduma ya HSI,VolP na IPTV, siyo tu kwa kujifunza kwa nadharia  bali pia ameweza kuitumia kwa vitendo.


Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Huawei, Jimmy Liguo alisema "Programu ya Seeds for the Future" inaendeshwa ulimwenguni kote. Miongoni mwa miradi ambayo Huawei imeipa kipaumbele ni huo na itaendelea kuwekeza kwa muda mrefu kwenye programu hiyo.

"Programu hiyo ilianzishwa na Huawei mwaka 2008 kwa lengo la kukuza uelewa katika masuala ya TEHAMA,  kuimarisha sekta ya mawasiliano, kuhamasisha ushiriki katika jamii ya kidijitali," alisema.


Mwaka 2008 Huawei ilizindua programu kuwaendeleza wataalamu ambao wanahitajika kwa haraka ili kuendeleza sekta teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi ambazo Huawei inafanya kazi zake. Huawei imeazimia kuwezesha mafunzo ambayo yataimarisha elimu inayotolewa darasani iendane na mahitaji halisi katika sekta ya TEHAMA ili elimu hiyo iwe endelevu.

Alisema katika nchi nyingi, bado kuna tatizo la mafunzo yanayotolewa hayaendania na kile kinachohitajika katika soko la ajira ulimwenguni, Hivyo watu wenye ujuzi wanatakiwa kupewa fursa za mafunzo zaidi ili kuweza kuitumia teknolojia ya kisasa.Kupitia Mradi wa Seeds for Future" Huawei imewezesha kutatua tatizo hilo.

No comments: