Droo
hii ya aina yake yawafanya watanzania 20 kuwa milionea leo! Wateja wa
tusker hadi leo wamepokea kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni 50
kwenye promosheni inayoendeswa na kampuni ya serengeti kupitia bia ya
Tusker iitwayo TUSKER FANYA KWELI NA UWINI.
Tayari
washindi 30 walikwishapatikana na wote wamepata zawadi zao za pesa
taslimu. Droo ya leo ambayo ilikuwa ya kusisimua ilikuwa tofauti na droo
zingine kwani leo washindi ishirini walitangazwa na sio kumi kama
ilivyozoeleka.Promosheni hii imeweza kupata washindi kutoka mikoa
mbalimbali na washindi wote wamekubali kwamba maisha yao yamebadilika
kwa njia moja au nyingine.
Wiki
iliyopita alipatikana mshindi Bw Albert Tarimo ambaye alionyesha kwa
furaha ujenzi wake na kusema kwamba atatumia pesa aliyopata kuweza
kuongeza matofali, dhahiri kuwa promosheni hiii imemfanya bw. Albert
afanye kweli katika harakati zake za ujenzi.
Kuna
ambao wamekiri kutumia pesa hizi kwa kulipa ada na wengine kuongezea
mtaji kwenye biashara zao. Droo za Tusker fanya kweli uwini zinafanyika
kila ijumaa katika studio za ITV na kushuhudiwa na afisa wa bodi ya
bahati nasibu ya taifa na wadau wengine, huku kipindi hiki kikirushwa
itv siku hiyo hiyo ya ijumaa jioni.
Baadhi
ya washindi wa droo hii ya nne ni Grace Richard kutoka Dar Es salaam,
Kitula kutoka Kahama shinyanga, Martina Japhet kutoka Tabora, J J
Malunga kutoka Shinyanga, kutoka mwanza Mr Isaya Stanley Furaha
Mushumbuzi kutoka Morogroro, Ibrahim Faiko kutoka Iringa, Victor Mwingo
kutoka Pwani . Washindi wote ishirini walipatikana kwenye simu na
walionyesha furaha isiyo na kifani. Walipewa maelekezo jinsi ya kupata
hela yao na ili kukamilisha ushindi wao. Washindi wote hukabidhiwa pesa
yao katika hafla fupi kila ijumaa huku wakiendelea kuburudika na tusker
na burudani kemkem.
Bado
kuna zaidi ya million hamsini za kushindaniwa kwa wateja wa tusker.
Tangu uzinduzi wa kampeni hii wapenzi wa tusker pamoja na kujishindia
pesa taslimu pia wameweza kujipatia zawadi nyingi zikiwemo bia za bure
za tusker, tshirt na kofia pamoja na kupata burudani maalum.
Akiongea
kwa furaha, meneja wa Masoko Nandi Mwiyombela amesema kwamba kwa sasa
promosheni inaendelea vizuri sana na wameweza kufikia malengo. “Pesa
taslimu ina nguvu. Kwa kiingereza wanasema ‘Cash is a strong tool’ na
kulingana na yale tunayosikia kutoka kwa washindi wetu tumegundua ya
kwamba kwa kweli kuwa na zawadi ya fedha taslimu ilikuwa uamuzi mzuri na
kwa uhakika wameelezea kuweka au kutumia pesa zao vizuri. Jambo
lililotusukuma mpaka kuamua kupata washindi ishirini na sio kumi kwa leo
ni kutokana na hamasa tunayopata kutoka kwa washindi wetu. Washindi
wanatokea mikoa mbalimbali, hilo ndilo lengo letu kubwa, kupata
washiriki na washindi nchi nzima.”, alisema Bi. Nandi.
“Tusker
Fanya Kweli Uwini’ inaendelea, pamoja na washindi ishirini tuliowapata
leo mpaka kufikia washindi 50. Tumeshatoa pesa taslimu shilingi milioni
50 na sasa imebaki milioni 50. Pia kama, mnanavyojua promosheni hii pia
inawazawadia wahudumu wanaohudumia wateja wetu, hadi kufikia leo
tumeweza kuwapatia shilingi milioni 22.” kamalizia Bi. Nandi.
Mteja
wa tusker anaruhusiwa kushiriki mara nyingi awezavyo, amepatikana mteja
aliyeibuka mshindi kwa mara ya pili katika hii promosheni ambayo
haiendeshwi kwa njia ya kompyuta bali kwa kuchanganya kuponi zilizojazwa
na watumiaji wa tusker na kuweza kupata majibu sahihi papo hapo.
Mkaguzi
kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Madam Chiku (katikati)
akihakiki taarifa za washindi 20 wa droo ya nne,kulia kwake ni Joseph
Silumbe - Visibility Manager na kushoto kwake ni Meneja wa bia ya Tusker
Jasper Migambile.
SBL
Visibility Manager Joseph Silumbe (kulia) akichezesha droo ya nne huku
akishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini
Madam Chiku (katikati) pamoja na meneja wa bia ya Tusker Jasper
Migambile (kushoto).
SBL
Visibility Manager Joseph Silumbe (kulia) akimpa kuponi ya mshindi
mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini madam Chiku
(katikati) huku akishuhudiwa na Meneja wa bia ya Tusker Jasper Migambile
(kushoto).
No comments:
Post a Comment