Na Mwandishi Maalum, New York
Rais Mstaafu wa awamu
ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema,
ingawa idadi kubwa ya vijana
wasiokuwa na uhakika wa maisha yao wala
kazi zenye tija na staha wapo katika nchi zinazoendelea, dunia katika ujumla
wake inapashwa kuonyesha utashi wa kisiasa na udhubutu wa kuwekeza kupitia vijana.
Amesema, mazingira
ya mamilioni ya vijana kukaa bila
shughuli ya aina yote kunatoa mwanya kwa vijana hao kurubuniwa
na kutumiwa na watu wasiokuwa na
nia njema na hivyo kutishia hali ya Amani, usalama na ustawi wa mwanadamu na hatimaye
kushindwa kufikia au kupata faida za kidemografia na maendeleo endelevu.
Mhe. Kikwete
ameyasema hayo jana ( jumanne) hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wakati alipotoa mhadhara wa 13
wa kumbukumbu ya Rafael M. Salas. Mhadhara huu
ambao mada yake ilikuwa ni “ kuwekeza kwa vijana ili kupata
faida ya kidemografia na maendeleo endelevu” uliandaliwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa kuhusu
Idadi ya Watu( UNFPA) ikiwa ni sehemu ya
mikutano ya mwaka ya Bodi za Mashirika na Mifuko iliyopo chini ya Umoja wa Mataifa.
Miongoni wa
viongozi waliohudhuria na kushiriki mhadhara ni
pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, na Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin , Bi. Carmelita R. Salas ambaye ni Mjane
wa Bw.
Rafael Salas aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
kwanza wa UNFPA, Mabalozi na
wataalamu mbalimbali.
“Tafiti na taarifa
mbalimbali zikiwamo za Umoja wa Mataifa, zinaonyesha wazi ongezeko la
idadi kubwa ya vijana
wanaokadiriwa kufikia 1.8 bilioni
idadi ambayo ni hazina na raslimali kubwa, lakini pamoja na uwingi wao, wengi bado wanaishi
katika hali ya umaskini uliokidhiri, na
ukosefu wa fursa mbalimbali ambazo zingewazesha
kuishi maisha yenye staha”.
akasema Kikwete
Na kuongeza kuwa,
kati ya vijana hao 1.8 bilioni, 74 milioni hawana ajira
akiwaelezea kama vijana wanaosubiri treni kando ya reli, treni ambayo haiji. Mazingira haya yanadhihirisha upotevu wa raslimali kubwa ambayo imewekezwa kwa vijana
hao na ambao wamepoteza matumaini.
Akafafanua zaidi kwa
kutoa takwimu mbalimbali zinazoonyesha tofauti
ya faidia za kidemografia kati ya mabara ya Ulaya, Asia, Amerika ya
Latini na Afrika ikiwa ni pamoja na utofauti wa matumizi ya raslimali watu kwa
nchi zile ambazo zimethubutu kuwekeza kwa vijana.
Rais Mstaafu Kikwete
katika mhadhara wake huo na ambao ulipokelewa vema sana na wajumbe waliohudhuria,
pia ametoa vielelezo vya kitakwimu
vinavyoainisha namna gan
bara la Afrika lilivyo nyuma
karibu katika ikielemewa kila
eneo kuanzia upatikanaji na utoaji wa huduma za uzazi salama, idadi ya wakunga wenye elimu ya kutosha,
upatikanaji wa huduma za afya,
elimu, maendeleo ya kijamii na
yenye tija na stahiki na kiwango cha matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango.
“Vijana wakiwezeshwa, wakiaminiwa, wakipewa fursa na wakithubutishwa wanauwezo
mkubwa sana wa kuleta mabadiliko. Tunatakiwa
kuwaamini, tunatakiwa kuwashirikisha na kusizisikia sauti zao” amesema.
Na kuongeza kuwa ,
mipango na sera zinazoandaliwa kwaajili
yao vijana ni vema zikawa
shirikishi na kuzingatia mawazo,
maoni na matakwa ya vijana.
“ Haya na mengi mengi yakitekelezwa kwa kuzingatia
mazingira ya kila nchi na vipaumbele
vyake, tunaweza kugema nguvu kazi hii
kubwa kujiletea maendeleo endelevu pasipo kumwacha yeyote nyuma” akasisitiza Rais Mstaafu.
Katika hotuba
yake hiyo iliyosheni takwimu na utafifi wa kisayasi, siyo tu kwamba imeainisha hali halisi ya mazingira waliyomo vijana bali pia
imechochea majadiliano na takafuri ya kina.
Baadhi ya mambo ambayo ameyatilia mkazo ni pamoja na umuhimu wa
jamiii kuzingatia uzazi salama na wa mpango na kuwa na idadi ndogo ya
watoto na ambayo wazazi wataweza kuimudu na elimu itakayokidhi mahitaji ya soko la ajira
lishe bora na uchumi imara na
endelevu.
Akimkaribisha Rais
Mstaafu kuzungumza, Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa Jan Elliason pamoja na mambo mengine
alimwelezea Mhe. Kikwete kuwa ni kiongozi mpenda amani na aliyemstari wa mbele katika kusimamia afya ya mama na mtoto.
No comments:
Post a Comment