Monday, June 27, 2016

SOBER HOUSE YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPIGA VITA MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA KULEVYA.

 Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kulia ni Mkuu wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji.
 Mkuu Wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House, Al-Kareem Bhanji aki akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kushoto ni Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga.
 Wananchi wakifatilia mada mbalimbali  kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
 Waathirika wa Dawa za Kulevya akiandamana siku ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
 Maandamano yakeendelea.
 Kikundi cha Sana cha Bagamoyo wakiigiza kama Waathirika wa Dawa za Kulevya.
 Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga akiwa kwenye picha ya  Waathirika wa Dawa za Kulevya.
Mkuu Wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji  akiwa kwenye picha ya  Waathirika wa Dawa za Kulevya
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Kituo cha Usaidizi Wa Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope Bagamoyo Sober House leo,June 26,2016 kimeadhimisha siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka June 26 lakini kwa Mwaka huu Kituo cha Sober kimeadhimisha siku hiyo Wilayani Bagamoyo.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo,Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga amesema vita vya Mapambano ya Dawa za Kulevya si vya Serikali pekee wala vya mtu mmoja bali ni vita vya kila mtu,ambaye anapaswa kuwajibika katika eneo husika ili kutokomeza kabisa uingizwaji Wa Dawa hizo.

Pia,Mkuu huyo Wa Wilaya ametoa wito kwa Viongozi Wa Dini ,Wananchi pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikiana kwa pamoja katika kutoa taarifa za kuwafichua waingizaji Wa Dawa hizo ili Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Amesema,Serikali imeahidi kupatikana kwa eneo kubwa ili kuendeleza kituo hicho na kuwasaidia vijana ambao ndio waathirika wakubwa Wa janga hilo na kuitaka jamii kuwatambua na kuwabaini waathirika wa Dawa hizo.

Kwa upande wake,Mkuu Wa Kituo hicho cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji amesema kituo hicho kimesaidia watu zaidi ya 100 mpaka sasa,ambapo ametoa Changamoto za ukosefu wa Majengo kituoni hapo  jambo ambalo limepelekea kwa sasa kulipa kodi kubwa ya pango.

Pia ameiomba Serikali kupatikana Ardhi ya kutosha ili kuweza kuongeza majengo na kukidhi haja ya kupokea Waathirika 200 ikiwa Wanaume 150 na Wanawake 50.

No comments: