Tuesday, June 28, 2016

SIMUTV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeondoa mashtaka mawili kati ya matano yaliyokuwa yanamkabili mbunge Tundu Lissu na wenzake watano kwa kosa la kuandika habari za uchochezi katika gazeti la Mawio; https://youtu.be/q9lNLM0watI

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika biashara kimataifa; https://youtu.be/4STkp4vmBkE

SIMU.TV: Wafanyabiashara wa soko la nguo Tandika wamelalamikia kitendo cha wafanyabiashara wadogo kupanga biashara zao barabarani kitendo kinachowafanya wao kukosa wateja; https://youtu.be/Np_nVKW6C8c

SIMU.TV: Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imeingia makubaliano na kampuni ya Saruji ya Simba Cement ili kuwezesha wateja wake kulipia kwa njia ya M-Pesa;https://youtu.be/Z2YidImTte4

SIMU.TV: Wananchi wa mtaa wa Kisiwani huko Songea wameelezea furaha yao kwa uongozi wa manispaa hiyo baada ya kutengenezewa barabara ambayo ilikua kero kubwa;https://youtu.be/bmIGdozLZwA

SIMU.TV: Benki ya Watu wa Zanzibar leo imetimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake huku matarajio yake makubwa ikiwa ni pamoja na kuwezesha wananchi katika mikopo nafuu na uchumi; https://youtu.be/jAwO4kAWY4M  

SIMU.TV: Kuwepo kwa vita ya wenyewe nchini na ulaji wa nyama ya Sokwe Congo DRC kumepelekea idadi kubwa ya watalii kuja nchini Tanzania kutazama Sokwe hao;https://youtu.be/9Zkb9fGRGE4

SIMU.TV: Kampuni ya simu za mkononi Tigo imezindua kampeni mpya ya Tigopesa, huduma itakayowawezesha wananchi kufanya miamala ya pesa kwa mitandao yote ya simu; https://youtu.be/bSkDuC2cMS4

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga imeendelea kupata matokeo mabaya katika michezo yake ya kimataifa baada yah ii leo kupoteza mchezo wake dhidi ya TP Mazembe kwa goli moja kwa bila; https://youtu.be/MPtCBcONx3Y

SIMU.TV: Waziri wa habari sanaa na michezo Nape Nnauye amesema moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wachongaji wa vinyago ni uwepo wa tozo kubwa pindi wanapojaribu kutafuta soko nje ya nchi; https://youtu.be/uK-YBFkjvnQ

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Temeke ambae ameteuliwa kuongoza wilaya ya Ilala Bi Sofia Mjema amewashauri wanachama wa klabu za Simba na Yanga kuyatumia matawi yao kujikwamua kiuchumi; https://youtu.be/TfheZB_HZ0k

SIMU.TV: Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imewasimamisha watendaji wake kumi na mbili kwa madai ya kuhusika na upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 571.https://youtu.be/-9MMxukQjhc

SIMU.TV: Waziri wa fedha na mipango amewasilisha bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma ambao umetajwa kunufaisha kampuni za ndani katika kupata zabuni. https://youtu.be/L6S-h6gZVls

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi wa eneo la Bunju B jijini Dar es salaam wamelalamikia uchafuzi wa mazingira unaofanywa na chuo cha usimamizi wa mazingira kilichopo eneo hilo.https://youtu.be/zwv7GSb5Ufc

SIMU.TV: Rais wa Comoro amesema kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na kukukuza uhusiano wake na serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali kama elimu afya na biashara. https://youtu.be/ClWy9UACXi4

SIMU.TV: Shirika la utangazaji la taifa TBC na shirika la mawasiliano nchini yametiliana saini katika mkataba wa milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa studio mpya za redio katika masafa ya FM. https://youtu.be/lNjDkLWsehg

SIMU.TV: Kikao maalum cha wakuu wa nchi na serikali  katika ukanda wa SADC kimeanza leo katika nchini Botswana kujadili namna ya kurejesha amani nchini Lesotho.https://youtu.be/ygUiVa-SkJI

SIMU.TV: Waziri wa habari sanaa na michezo amemteua Dr Hubert Makoye kuwa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo TASUBA.https://youtu.be/mCGzEx2VXDY

SIMU.TV: Jamhuri ya watu wa Czech imeotoa faru mmoja ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali kurejesha faru weusi nchini. https://youtu.be/57s9NJvfMaQ

SIMU.TV: Zaidi ya kampuni 2300 za ndani na nje ya nchi zinatarajia kushiriki katika maonesho ya biashara ya kimataifa ya sabasaba. https://youtu.be/9W6FtmJY18A

SIMU.TV: Taasisi ya ukuzaji wa sekta ya fedha nchini imezindua mfuko wa kuwezesha kampuni za bima nchini kubuni bidhaa za bima kwa upande wa kilimo na afya.https://youtu.be/QkRulNA_m-4

SIMU.TV: Bei ya baadhi ya mazao ya vyakula  katika soko la kariakoo jijini Dar es salaam imeshuka kutokana na upatikanaji wa mazao hao kuongezeka.https://youtu.be/EoEh73pfMvM

SIMU.TV: Mamlaka ya chakula na dawa TFDA ikishirikian ana mamlaka ya mapato  TRA kanda ya ziwa zimeteketeza shehena ya bidha za dawa na vipodozi katika wilaya ya Geita.https://youtu.be/ESioVd_glKE

SIMU.TV: Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya helium imegunduliza nchini katika eneo la bonde la ufa ambapo itakua ikipatatikana hapa nchini tuu. https://youtu.be/qq4FG6q_JTQ

SIMU.TV: Mabingwa ya ligi kuu nchini timu ya Yanga wameshindwa kutamba uwanja wa taifa baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka kwa timu ya Tp Mazembe kwenye mchezo wake wa kombe la shirikisho barani Afrika.https://youtu.be/zdqM1Mh1YP8

SIMU.TV: Baadhi ya Mashabiki wamemuomba mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kuacha tabia ya kuwaingiza bure mashabiki kwa sababu mashabiki halali hawapati nafasi ya kuingia uwanjani. https://youtu.be/tHaX9YYmlI0

SIMU.TV: Wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo imedhamiria kushirikiana na wizara ya ardhi na makazi kutatua mgogoro wa kiwanja cha wasanii wa sanaa ya uchongaji. https://youtu.be/S9GpIYEpenQ

SIMU.TV: Mwanariadha mkongwe Mzaeli Kiyoma ameishauri serikali kutumia wanamichezo wakongwe ili kuweza kuinua sekta ya michezo nchini.https://youtu.be/L5BJ3gNVavo

SIMU.TVKocha mkuu wa timu ya taifa ya England ametangaza kujiuzulu kuifundisha timu ya hiyo baada ya kuondolewa kwenye michuano ya EURO 2016.https://youtu.be/GypwJOxWr54

No comments: