Tuesday, June 7, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wakazi wa mkoa wa Tabora na Katavi wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa daraja la mto Kogo ambalo limesababisha kupanda kwa gharama za usafiri.https://youtu.be/-w-6BOuraX8

SIMU.TV: Hali ya upatikanaji wa sukari katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam bado hairidhishi kutokana na bidhaa hiyo kuendelea kupatikana kwa mashaka na kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi. https://youtu.be/LabHNom1NMI

SIMU.TV: Rai amemteua jaji Ferdinandi Wambali kuwa jaji kiongozi na kuchukua nafasi iliochwa na jaji Shaban Lilaaliyeteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya rufani.https://youtu.be/7fSz9WhdSXo

SIMU.TV: Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limewatawanya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  waliokaidi agizo la polisi la kutofanya mkusanyiko. https://youtu.be/wBmmbsO0_70

SIMU.TV: Jeshi la polisi nchini limepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na vyama vya siasa baada ya kugundua yanampango wa kuvuruga amani ya nchi. https://youtu.be/VX2Ehh1xvQ0

SIMU.TV: Idadi ya abiria wanaohudumiwa na  Swiss port kampuni ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwenye ndege imeongezeka kutoka laki tisa hadi zaidi ya milioni moja kutokana  na kukua kwa shughuli mbalimbali za uchumi nchini. https://youtu.be/1gUxA93AGdc

SIMU.TV: Vijana saba wamehitimu mafunzo ya kwanza ya ufundi stadi  visomo kwa njia ya simu yanayotolewa na mamlaka ya ufundi stadi nchini VETA.https://youtu.be/5dUDxzDXGak

SIMU.TV: Wataalamu wa mboga kutoka kampuni ya Matayo ambayo inajishughulisha na kilimo cha mboga imesema wananchi wa mkoa wa Mara wanaweza kuondokana na umaskini kwa kujishughulisha na kilimo cha mboga mboga. https://youtu.be/EQI4IkZVulY

SIMU.TV: Sekta binafsi na mashirika ambatano zimehimizwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa taifa wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano.https://youtu.be/DN82QdNpevI

SIMU.TV: Tume ya taifa uchaguzi NEC imekabidhi shilingi bilioni kumi na mbili zilizobaki kwenye uchaguzi mkuu wa rais wabunge na madiwani mwaka jana.https://youtu.be/4MhQzbLZ2IM

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amepokea madawati mia moja yaliyotolewa na umoja wa mafundi geraji kutoka eneo la Tegeta. https://youtu.be/Pog1BhRf_kk

SIMU.TV: Wafanyabiashara wa soko kuu la manispaa ya Lindi wametakiwa kuacha tabia ya kutafuta faida kubwa kwa kupandisha bei ya vyakula kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. https://youtu.be/FXTHs9bStiA

SIMU.TV: Serikali ya Saudi Arabia imekabidhi tani 100 za tende ikiwa ni mpango wa kuwasaidia waislamu wanaofunga nchini. https://youtu.be/Y1c8eAOnKfY

SIMU.TV: Mpango wa taifa wa damu salama nchini umejipanga kukusanya chupa za damu laki tatu katika kuelekea maadhimisho ya siku ya damu salama duniani.https://youtu.be/wCb-uq2mMBU

SIMU.TV: Mahakama ya Mwanzo ya manispaa ya kinondoni imewapandisha kizimbani watuhumiwa waliotumia vibaya barabara za magari yaendayo haraka kinyume na sheria.https://youtu.be/U-2cod_2NCI

SIMU.TV: Chama kikuu cha wakulima wa tumbaku mkoani Katavi  kimepongezwa kwa kuonyesha kwa vitendo uwekezaji kwenye majengo ya kibiashara.https://youtu.be/UPOfHSLb3AM

SIMU.TV: Watanzania wamehamishwa kulima zao la mchaichai baada ya kugundulika kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi. https://youtu.be/dQg3aGqvHAs

SIMU.TV: Jumuiya ya kibiashara ya Marekani American chamber of commerce imetialia saini  na benki M katika kuboresha na programu ya Daraja la mafanikio kwa vijana.https://youtu.be/VRGL5MBEOeA

SIMU.TV: Shirikisho la soka TFF limekubali yaishe kuhusiana na uamuzi wa Klabu ya Yanga wa kusimamia uchaguzi wake wenyewe. https://youtu.be/HSIBDxdnS1M

No comments: