Sunday, June 19, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Serikali imewataka wakazi wa wilaya za Chemba na Kondoa kuacha kushutumia kutiliana sumu juu ya ugonjwa ulioibuka juzi na badala yake waiachie wizara ya afya ifanye uchunguzi wake; https://youtu.be/Tk61bUpTk0g

SIMU.TV: Jeshi la polisi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga linamshikilia bwana mmoja kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa kike na kumsababishia maumivu makali;https://youtu.be/50Lg8S9h9NY

SIMU.TV: Kijana wa kitanzania Ismail Kambi ameibuka mshindi wa kusoma Quran na kujishindia zawadi ya gari aina ya Noah yeye thamani ya shilingi Milioni 14;https://youtu.be/lwyOJ80xsSQ

SIMU.TV: Watumiaji wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es salaam kuanzia kesho wataanza kutumia tiketi za kielekitroniki ili kurahisisha matumizi ya mabasi hayo;https://youtu.be/Z4XkbASHwKw

SIMU.TV: Chama cha UDP kimemuomba Rais Magufuli kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya vyama siasa ili kuweza kukuza Demokrasia; https://youtu.be/Khozy-sLkz8  

SIMU.TV: Kikosi kamili cha Yanga kutoka nchini Tanzania kilichopo nchini Algeria hivi sasa kinatarajia kushuka dimbani usiku huu hapo baadae na wenyeji wao Mo Bejaia katika michuano ya shirikisho barani Afrika; https://youtu.be/IBzIVKHdV-g

SIMU.TV: Maendeleo ya mchezo wa Golf nchini yatapatikana endapo watanzania kwa umoja wao wataamua kuelekeza nguvu zao katika mchezo huo; https://youtu.be/r8-Revm2zho

SIMU.TV: Wasanii maarufu wa kuimba na kuigiza kutoka Marekani na India wanatarajia kupamba jukwaa visiwani Zanzibar katika utoaji wa tuzo za ZIFF;https://youtu.be/pRhYC9fYdz4

SIMU.TV: Serikali imewataka watanzania kushiriki mazoezi mbalimbali ili kuwawezesha kuweka miili fiti kiafya na kuepukana na mgonjwa yasiyo ya lazima;https://youtu.be/26170nh8_g0

SIMU.TV: Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema watu waliofariki kwa ugonjwa usiojulikana katika Wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma imefikia saba. https://youtu.be/vmt4ONTIix0

SIMU.TV: Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema serikali ina mpango wa kuajiri wataalamu wa afya ili kuondoa changamoto ya upungufu wa madaktari. https://youtu.be/Uw_KZlCTAxU

SIMU.TV: Waziri wa maliasili na utali Profesa Jumanne Maghembe amesema serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za shirika la hifadhi nchini  TANAPA katika kukabiliana na ujangili. https://youtu.be/Y7n-_qgCu7w

SIMU.TV: Wakulima wa zao la shaiyiri katika mikoa ya Arusha na Manyara wameiomba serikali kuwapunguzia gharama za viwatilifu na mbolea ili wawezekumudu kilimo hicho.https://youtu.be/oHPejokC8Ds

SIMU.TV: Wakulima wa korosho kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wamelalamikia kucheleweshwa kwa ugawaji wa pembejeo za ruzuku. https://youtu.be/-iWCKIfPgq8

SIMU.TV: Jumla ya kaya 915 katika mkoa wa Kagera zimeondolewa katika mpango wa kunusu kaya masikini baada ya kuonekana hazikidhi vigezo vya kuendelea kuwa katika mpango huo. https://youtu.be/pC9s7nMz4Bs

SIMU.TV: Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi amewataka watanzania kushirikiana bila kujali itikadi zao ili kulinda amani ya nchi. https://youtu.be/1qbl7p0LgPY

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi kuhakikisha wanawapa watoto wao elimu ili kuwawezesha kujenga misingi bora katika maisha.https://youtu.be/O1kZG0CyiZw

SIMU.TV: Watanzania wameaswa kudumisha amani iliyoko nchini kwa kujiepusha na matukio ya uvunjifu wa amani. https://youtu.be/wwMxdWpizjo

SIMU.TV: Klabu ya Yanga leo usiku inaingia uwanjani huko Algeria kucheza mchezo wa makundi ya kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaiya ya huko nchini Algeria.https://youtu.be/s-RZbyYIG5Q

SIMU.TV: Waziri wa habari sanaa na michezo ameshiriki katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya Yoga na kuwataka watanzania kudumisha tamaduni zao kama wahindi walivyofanya kuitunza Yoga. https://youtu.be/OKghkkTFSGg

SIMU.TV: Licha ya TFF kufuta uchaguzi wa chama cha michezo cha Kinondoni KIFA uongozi uliochaguliwa umeendelea na kazi kama kawaidana kusema hawajapata barua ya TFF.https://youtu.be/HOakBpeMls0

SIMU.TV: Kamati ya utendaji ya chama cha kuogelea imesema watakutana ili kujadili ratiba ya kushiriki mashindano ya Olimpiki. https://youtu.be/Wnuj1tqjApY

SIMU.TV: Timu ya Ureno imefikisha alama mbili katika mashindano ya EURO baada ya kutoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Austria hapo jana usiku.https://youtu.be/brjbBCQJJtU

No comments: