Tuesday, June 14, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Serikali imezitaka halmashauri, mikoa na wilaya kutambua kuwa jukumu la kukusanya damu salama ni la kwao na wizara haitahusika tena na jukumu hilo;https://youtu.be/il0rcJl7LmE

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Mahina wilaya ya Nyamagana wameandamana mpaka ofisi za CCM wilayani humo kwa lengo la kujua hatima ya Meya wao anayetishiwa kufa;https://youtu.be/Oxraj2crQdg

SIMU.TV: Benki ya CRDB imetoa jumla ya shilling Milioni 375 katika kuchangia tatizo la madawati nchini kama njia ya kuunga mkono jitihada za Rais;https://youtu.be/FqjZ3FR44t8

SIMU.TV: Jamii ya singasinga wanaoishi hapa nchini wametoa msaada wa vifaa katika sekta ya afya baada ya kusaidia magodoro 100 kwa wilaya ya Ilala;https://youtu.be/ITdnU16Zq_g  

SIMU.TV: Waziri wa nchi TAMISEMI  George Simbachawene amewataka wawekezaji nchini kuweka mazoea mazuri na wananchi wanaozunguka maeneo hayo ili kuleta maendeleo  kwa wananchi hao; https://youtu.be/dK6re8DUdDU

SIMU.TV: Wananchi wanaozunguka mgodi wa Kata Mkoani Mara wameanza kunufaika na mradi huo baada ya kuanza kufanya shughuli zake za uchimbaji;https://youtu.be/0IchwwMq1jQ  

SIMU.TV: Waziri Simbachawene amesema bado serikali inathamini michezo licha ya kusitishwa kwa mashindano ya Umitashunta na Umisseta kupisha matengenezo ya madawati; https://youtu.be/BCc-dEFIjKM

SIMU.TV: Timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys imeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Shelisheli katika mashindano ya kuwania kufuzu AFCON kwa vijana; https://youtu.be/ZmG-FR-t3ZA

SIMU.TV: Timu ya Kikapu ya Cleveland Cavaliers imeharibu sherehe ya Ubingwa ya Golden States Warriors baada hapo jana kuwafunga wakali hao wa NBA;https://youtu.be/HQ_Dg7XXw3I

SIMU.TV: Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa amewakumbusha watanzania kufanya kazi kwa bidii. https://youtu.be/3tv4kArcUxs

SIMU.TV: Nyumba zilizojengwa na wavamizi katika kiwanja kinachomilikiwa na shirika la utangaji TBC zimebomolewa baada ya wananchi hao kugoma kuondoka.https://youtu.be/xpVI9j74NO4

SIMU.TV: Waziri wa elimu sanyansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezindua taarifa ya utafiti wa kuhusu kiwango cha wanafunzi kujua kusoma kuandika na kuhesabu.https://youtu.be/QCO3dmtpLhw

SIMU.TV: TCRA imesema ni kosa kisheria kwa mtumiaji wa simu za mkononi kubadilisha namba tambulishi za simu yaani IMEI kutoka simu moja kwenda nyingine.https://youtu.be/yMqBPb-ovT4

SIMU.TV: Sekretariati ya chama cha TLP imeeleza kushangazwa na baadhi ya watu kusema kuwa rais Dr. John Pombe Magufuli  anatawala bila kuzingatia demokrasia na sheria.https://youtu.be/e8Dv9p_JJ1I

SIMU.TV: Waziri mkuu mstaafu Dr. Salim Ahmed Salim amewataka vijana nchini kujua historia ya nchi yao na kudumisha ushirikiano na nchi nyingine kwa maendeleo ya bara la Afrika. https://youtu.be/zl4sUBmVCxI

SIMU.TV: Waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee jinsia na watoto amesema jukumu la kuchangia damu ni la halmashauri na sio la wizara peke yake.https://youtu.be/O8Bcg8CJ6lQ

SIMU.TV: Kiwanda cha uzalishaji wa sukari cha TPC kilichopo mkoani Kilimanjaro kimeanza uzalishaji wa sukari baada ya kusitisha kwa muda wa miezi mitatu.https://youtu.be/dyilOZZxB5o

SIMU.TV: Kampuni za uwekezaji zikiwemo zile za madini zimetakiwa kushirikiana na wananchi wa maeneo waliowekeza ili kuepusha migogoro kati ya wawekezaji na wananchi. https://youtu.be/XLf6s-R6qPI

SIMU.TV: Benki ya CRDB imechangia juhudi za kumaliza tatizo la madawati kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni mia moja https://youtu.be/R4_yLJorC-w

SIMU.TV: Benki ya Exim imetumia zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii kwa mwaka huu. https://youtu.be/ag-eaoJpL4E

SIMU.TV: Chama cha waongozaji wa watalii nchini kimeomba serikali kuangalia namna ya kupunguza kodi kwa watalii ili kuvutia watalii zaidi. https://youtu.be/WZl8TDmCSoQ

SIMU.TV: Wachezaji 24 wameitwa kuunda timu ya vijana ya Serengeti boys ili  kujiandaa na michuano ya kufuzu mashindano ya Afrika kwa vijana. https://youtu.be/WwMHjsjxxcM

SIMU.TV: Vilabu vya ligi kuu Tanzania vimetakiwa kupeleka majina ya viwanja vitakavyotumia katika michuano ya ligi kuu msimu ujao ili vipewe leseni.https://youtu.be/pKj9Vb4B-Qc

SIMU.TV: Kampuni ya uzalishaji wa vinywaji baridi ya Cocacola imesema itaendelea kudhamini mashindano ya UMISETA licha ya mashindano hayo kuairishwa na serikali kupisha zoezi la uchangiaji wa madawati. https://youtu.be/SnLvCjkShnY

SIMU.TV: Kamati ya muda inayosimamia uchaguzi wa klabu ya Stand United imewasimamisha kazi viongozi wa wawili wa klabu hiyo. https://youtu.be/_L2JWP-uARs

No comments: