Friday, June 17, 2016

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASHEREKEA MIAKA 10 YA USAFIRI WA ANGA KWA KUONGEZA SAFARI MPYA QATAR.

· Safari tano kwa siku ikiwamo za alfajiri kwa wasafiri wote wa Abu Dhabi na Qatar

· Nyongeza ya safari za jioni kwa kipindi za kiangazi ikiwa ni maalumu kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaoenda kutembea

Shirika la Ndege la Etihad limesherehekea miaka 10 ya huduma ya usafiri wa anga kwa kuzindua safari tisa za ndege kutoka Abu Dhabi – Doha kipindi hiki cha kiangazi ikitimiza ahadi yake kuwa shirika bora la usafiri katika ukanda huo wa Gulf kibiashara.

Kuanzia 1 Agosti 2016 shirika hili litaongeza safari za wiki kuelekea mji mkuu wa Qatar. Safari mpya za ndege za alfajiri pamoja na jioni siku ya Alhamisi na Jumamosi zitawawezesha wasafiri ambao ni wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati kati ya Abu Dhabi na Doha.

Safari hizo mpya zitawawezesha wasafiri kutoka Doha kuwa na chaguo la usafiri wa ndege za Shirika la Etihad zinazofanya safari zake maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati, Ulaya, Afrika, Asia, na Amerika Kaskazini.Huduma hiyo mpya inaendana na kipindi hiki cha miezi ya kiangazi ambacho huwa na ongezo idadi ya wasafiri.

Tangu kuanzishwa safari za Doha mwaka 2016, Shirika la Ndege la Etihad limekuwa likiboresha huduma zake ili kuendana na mahitaji halisi ikiwamo kuiunganisha dunia na huduma mbalimbali zinazopatikana Abu Dhabi.

Makamu wa Rais wa Masoko katika Shirika la Ndege Etihad, Daniel Barranger alisema, “Qatar ni kitovu cha biashara kwa Shirika la Etihad. Tangu 2006 kumekuwapo maendeleo mazuri ya safari za ndege nne kwa siku kati ya Abu Dhabi na Doha, ndiyo sababu tunasherehekea kumiza miaka 10 kwa kuunganisha miji hii mikuu miwili kwa kuongeza safari za ndege tisa kila wiki ikiwa ni kuonyesha dhamira yetu kukuza biashara Doha.”

Aliongeza kuwa, “Kwa kuboresha safari zetu kwenda na kurudi Doha, tumejenga mtandao imara na ni matumaini yetu wateja wetu watakuwa na wigo mpana wa kuchagua usafiri muda unaomfaa kwenda Abu Dhabi.”

Wageni wanaosafiri kwenda Abu Dhabi watakuwa na fursa ya kupanga na kuchagua ndege aipendayo kufika Ulaya, ikiwamo miji ya London, Manchester, Paris, Dublin, Rome, Munich, Milan, Geneva, Madrid, Athens na Istanbul. Pia, Delhi, Mumbai, Kathmandu, Dhaka, Calicut, Cochin pamoja na Hyderabad miji inayounganisha India.

Pia mteja anaweza kusafiri kwa ndege ya shirika la Etihad kutokea Doha na kutembelea miji mbalimbali ya USA; – New York, Chicago, San Francisco, Los Angeles, Washington na Dallas.

Wasafiri pia watapata huduma ya kipekee ya US Pre-Clearance immigration and customs wakiwa katika uwanja wa ndende wa kimataifa wa Abu Dhabi.

Hii humwezesha msafiri anapowasili Marekani kama msafiri wqa ndani kumpuguzia muda ambao angetumia kushughulikia na kukamilisha. masuala ya uhamiaji na taratibu za kuwasili.

Safari za kila siku kati ya Abu Dhabi and Doha. Ratiba mpya ya usafiri wa ndege utakaoanza tarehe 1 Agosti, 2016.


No comments: