SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia kitengo cha cha vifurushi, limeanzisha safari mbili kwa wiki ili kusafirisha mizigo kwa kutumia ndege ya A330 itakayotoa huduma zake kwenda Uwanja wa Ndege Brussels nchini Belgium kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kiuchumi kati ya Abu Dhabi na Brussels na kongeza ufanisi wa huduma kwa wateja wake.
Ndege hiyo hutoa huduma ya usafiri mjini Brussels pia ikibeba mizigo, usafiri huo wa ndege ni muhimu kwa uchumi wa Belgium na Ulaya kwa ujumla.
Makamu wa Rais Kitengo cha Vifurushi wa Shirika la Ndege la Etihad, David Kerr alisema, “Brussels ni njia muhimu barani Ulaya kwa shughuli za usafiri wa ndege, ni eneo ambalo tumepanga kujitanua zaidi kwa mwaka huu, tunafurahia kuanzisha shughuli zetu ndani na nje ya mji huu. Brussels ni kiungo muhimu barani Ulaya na kiungo muhimu kwa Afrika, hivyo tunaamini itakuwa njia muhimu zaidi ambayo itaunganisha ulimwengu katika mtandao wa usafiri wa anga.”
Ikiwa ndiyo inaoongoza barani Ulaya kwa lango la kibiashara, Uwanja wa Ndege wa Brussels utanufaika zaidi na huduma ya usafirishaji wa mizigo kutokana na kuwapo na barabara ambazo haziwezi kustahimili usafirishaji wa mizigo kwa sababu ya kuharibiwa na barafu, jambo liloloweza kuharibuvifaatiba na bidhaa zingine zisizodumu kwa muda mrefu.
Kitengo cha Vifurushi Etihad kilizindua usafirishaji wa bidhaa za madawa ya hospitali Machi 2015. Kwa kuzingatia umuhimu wa bidhaa hizo zinahitaji umakini wa hali ya juu na husafirishwa kwa makubaliano na viwanda husika.
Kuwapo kwa vifaa maalumu vya kupima joto kumewezesha kudhibiti kiwango cha joto linalohitajika ili kuziweka dawa hizo katika ubora unaostahili ili kuendana na mazingira ya hali ya hewa vinaposafirishwa.
Programu hiyo inasimamiwa na wafanyakazi waenye uzoefu Kitengo cha Vifurushi cha Etihad huku wakisaidiana na wafanyakazi wengine.
Ndege hiyo mpya itakayosafirisha mizigo, itaunganisha masuala mbalimbali baina ya Abu Dhabu na mtandao wa wasafirishaji wengine ulimwenguni kukiwa na takriban fursa 1,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment