Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi
(katikati) na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba (kushoto) wakikata utepe ikiwa ishara
ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini
Dar es Salaam. Kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna
Jenerali, Thobias Andengenye.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi
akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuishukuru Serikali ya Japan kwa
kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari tisa kwa ajili ya kazi ya
kuzima moto na uokoaji nchini. Wa pili kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba
akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye.
Wa pili kulia ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatus Kipali na Kamishna Msaidizi,
Fikiri Salla. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye akitoa hotuba
fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi ili aweze kuzungumza na baadaye
kukabidhiwa magari matano ya kuzima moto na uokoaji. Magari hayo yametolewa na Serikali ya
Japan kupitia balozi wake nchini, Masaharu Yoshiba. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika nje
ya Jengo la Wizara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian
Mapfa (kushoto) akimkabidhi zawadi Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba, mara baada ya
Balozi huyo kuikabidhi Wizara hiyo msaada wa magari tisa ya kuzima moto na uokoaji. Tukio la
makabidhiano ya magari hayo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara, jijini Dar es Salaam leo.
Wakuu wa Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji pamoja na wageni waalikwa, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye
(hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kabla ya Serikali ya Japan kutoa msaada
wa magari tisa ya kuzima moto na uokoaji. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara, jijini
Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Andengenye aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada
mkubwa ambao wameutoa kwa Jeshi lake.
Sehemu ya magari tisa yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaharu Yoshiba kwa niaba ya
Serikali yake yakiwa nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Magari hayo
yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera
na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment