MFUKO wa kichocheo wa SAGCOT wasaini makubaliano ya utekelezaji wa Mradi na kampuni zilizoomba ufadhali wa Fedha kwaajili ya uimarishaji wa Viwanda pamoja na ukuzaji wa Kilimo hapa nchini jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo amesema kuwa Mfuko wa SAGCOT wamesaini mikataba kwaajili ya kibiashara kwanzia mtaji kati ya Dola Za Kimarekani milioni 50 hadi 100 zitakuwa zikitolewa kwa miradi kupitia madirisha ya Matching Grant Fund(MGF) ambao utakuwa ukitatua changamoto za wakulima na masoko yao.
Pia amesema kuwa dirisha jingine ni la Social Venture Capital(SVC) dirisha hili litalenga kuwzesha kujengwa kwa viwanda vikubwa ba vya kati ili kutoa masoko kwa wakulima hasa wa maeneo amayo yana mazao mengi lakini hakuna kiu ya sekta binafsi ya kuwekeza katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza na wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo hapa nchini jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, John Kyaruzi akizungumza na wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo hapa nchini jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwakaribisha wawakilishi wa wakulima kwenda kuelezea kazi zao mbele ya Mgeni rasmi kutoka wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji.
Mwenyekiti kampuni ya Cane Care Limited, Dr. George Mlingwa akifafanua jambo mbele ya Mgeni Rasmi na mwakilizshi wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Joel Malongo kuhusiana na kampuni yake ya Kilimo cha Miwa pamoja na hatua za uandaaji wa utengenezaji wa Sukari hapa nchini katika kiwanda chake Kidogo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na vongozi wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo (Mwenye tai nyekundu waliosimama) akisuhudia wawakilishi wa vyama vya wakulima wakisaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo katikati kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe na Katibu Mkuu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, John Kyaruzi wakiwa katika mkutano huo wa wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment